Waziri wa Michezo akijadiliana na ujumbe wa Elwada makubaliano ya ushirikiano kati ya Misri na Afrika Kusini katika uwanja wa kupambana na Madawa ya kulevya

 Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana jioni ya leo na ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Kupambana na Madawa ya kulevya  "Wada", uliowakilishwa na Mkurugenzi wa Ofisi ya kikanda ya Shirika hilo  Barani Afrika, Bwana Rodney Swiglar na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Programu za Kitaifa na Kikanda Bwana Tom May, na Bwana Khaled Gallant, Kaimu Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Kupambana na Madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.

 Mkutano huo ulijadili maendeleo ya makubaliano ya pamoja ya ushirikiano kati ya mashirika mawili ya kimisri na Afrika Kusini katika uwanja wa kupambana na utupaji macho, kwa mahudhurio ya Mhandisi Hisham Hatab, Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Misri.


 Dokta  Ashraf Sobhy alisisitiza kwamba michezo ya kimisri kwa sasa inashuhudia sifa kubwa sana na isiyo ya kawaida katika kiwango cha mashindano ya michezo, zote mbili kwa suala la kushiriki vyema katika vikao tofauti vya michezo ya kimataifa na kufikia matokeo yasiyotabirika au kwa upande wa kukaribisha Misri  kwa michuano tofauti na  shughuli za kitaifa na za kimataifa za michezo ,  linalofanyika  uwanja wa kupambana na Madawa ya kulevya ni moja wapo ya vipaumbele muhimu ambayo Wizara ya Vijana na Michezo inalipa kipaumbele kabisa, iwe kwa upande wa ushirikiano na shirika la kimataifa au mashirika ya kitaifa yanayohusika na kupambana na  Madawa ya kulevya katika nchi mbali mbali katika muktadha wa kuunda mazingira safi ya michezo yasiyokuwa na Madawa ya kulevya.


 Waziri wa Vijana na Michezo aliashiria  Uungaji mkono na  msaada kamili uliotolewa kwa Wizara kwa hatua zote zinazohusiana na kuendeleza utendaji wa kuzuia Madawa ya kulevya nchini Misri kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali za kimataifa zinazohusika.


 Katika muktadha huo huo, mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kupambana na  Madawa ya kulevya alisisitiza kwamba hivi sasa Misri  inashuhudia ustawi kwa michezo na maendeleo wa kushangaza katika suala la kukemea  Madawa ya kulevya,  itakayowakilisha nyongeza kubwa kwa ushirikiano na kubadilishana uzoefu kati ya Misri na Afrika Kusini katika suala hili.


 Mkutano huo ulihudhuriwa na Dokta Osama Ghoneim, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kupambana na Madawa ya kulevya la kimisri "nado" na Dokta Hana, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kimisri.

Comments