Morocco ishinda medali ya dhahabu ya kikapu ya wanawake kwenye Michezo ya kiafrika kwa Olimpiki ya walemavu
- 2020-01-29 21:39:29
Timu ya Morocco ya wanawake kwa mpira wa kikapu ilishika nafasi ya kwanza na medali ya dhahabu katika mashindano ya michezo ya kiafrika kwa Olimpiki ya walemavu , baada ya kuishinda mwenzake timu ya Misri katika mchezo wa fainali kwa 27-24 katika pambano la kwanza mnamo siku ya nne na ya mwisho ya mashindano.
Timu tano zinashindana katika mpira wa kikapu, nazo ni Misri, Morocco, Algeria na Tunisia, Burundi.
pambano hilo hufanyika kwa vipindi vinne, dakika 8 kwa kila kipindi , na kila timu inacheza na wachezaji watano.
Timu ya Wamisri inawakilishwa na: Mona Hatem, Nada Magdy, Yasmine Mohamed, Basma Mohamed, Hadir Ashraf, Heidi Yasser, Nada Ezzat, Mayada Adel, Maryam Hossam, na Menna Allah Karim.
Wakati timu ya Morocco inawakilishwa na : Fatima Abdel Rahman, Fatima Picchu, Iman Bouchan, Nadia Al-Khattab na Manal Al-Drissi na Sakina Abu Faris.
Comments