Waziri wa michezo akutana na balozi wa Jamhuri ya Koba ili kujadiliana mahusiano mawili kati ya nchi mbili
- 2020-02-01 23:33:00
Dokta Ashraf sobhy waziri wa vijana na michezo anakutana leo na Bibi " Tania Agear Fernandes" balozi wa nchi ya Koba kwenye Jamhuri ya Misri ya Kiarabu , na hivyo ili kujadiliana mahusiano ya pamoja kati ya nchi mbili katika sekta ya vijana na michezo .
Mkutano huu unakuja katika mfumo wa wizara ya vijana na michezo ili kugundua njia mpya za shirikiano na nchi za ulimwengu zote ili kupata faida ya maendeleo yanayokabilia dunia katika pande mbili vijana na michezo . Vilevile , kuenedana ujuzi unaolenga kutekeleza manufaa ya juu kutoka majarabio ya dunia yanayofaulu .
Na pande mbili zilichukua utafiti wa kusaini mkataba wa maelewano kati ya wizara na chuo cha kitaifa kwa michezo na mafunzo ya kimwili na viburudisho katika Jamhuri ya Koba
Katika upande huo huo , Waziri wa michezo alisema kuwa sisi tunalenga kuimarisha na kutoa msaada kwa shirikiano la kiufundi katika sekta za mafunzo ya kimwili na michezo ,akisisitiza kuwa ushirikiano huu utashiriki katika kubadilishana wajumbe , kocha na wataalamu katika kiwango cha michezo .
Sobhy aliongeza kuwa ushirikiano utajumuisha pia ziara kwa viongozi , kocha wakuu katika sekta ya usimamizi wa michezo na kuhukumu na kufanya mazoezi kutokana na vigezo na miundo ya usimamizi mpya ili kupata manufaa ya majaribio ya nchi mbili katika sekta huu .
Waziri wa michezo akiashiria kuwa mkataba wa maelewano utajumuisha kufanaya warsha wa pamoja kukusu maudhui ya " usimamizi wa michezo mpya unaokusanya usimamizi wa mizozo , matatizo na majaribio ya ufanisi katika kupambana na fujo ya viwanja , haki za kutangaza katika runinga , uwekezaji wa kimichezo na michezo ya waelemevu " .
Kwa upande mwingine , balozi wa Jamhuri ya koba alitoa shukrani kwa upokeaji mzuri , akisisitiza kuwa Misri ni nchi muhimu zaidi inayotarajiwa kushirikiana na koba hasa baada ya maendelezo ya kiuchumi na kisiasa yanayoshuhudia na Misri sasa hivi , akiashiria kuwa maendelezo haya yanajumuisha sekta ya michezo inayokawa mojawapo ya sekta muhimu zaidi ambayo misri inaitilia mkazo kama msaada mkubwa kwa uchumi wa kitaifa .
" Fernades " alionesha hamasa kubwa kwa mafanikio ya ushirikiano huo na utakaojumuisha kusaini mkataba wa maelewano kati ya chuo cha kitaifa cha michezo na mafunzo ya kimwili na viburudisho vya Jamhuri ya koba na wizara ya vijana na michezo ya Kimisri.
Dokta Ghada Hussin mkuu wa mahusiano ya nje na Rada Saleh mkuu wa mahusiano ya umma katika wizara ya vijana na michezo walihudhuria mkutano .
Comments