Mawaziri wawili wa vijana na michezo na mshikamano wa kijamii wanashuhudia sherehe ya hitimisho kwa michezo ya kwanza ya Kiafrika kwa Olimpiki ya walemavu
- 2020-02-01 23:39:00
Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo na Neven Alkabag Waziri wa mshikamano wa kijamii, jioni ya leo Alhamisi wameshuhudia hitimisho la michezo ya kwanza ya Kiafrika kwa Olimpiki ya walemavu iliyokaribishwa na Misri mnamo kipindi cha tarehe 23 hadi 31 mwezi huu wa Januari, chini ya uangalifu wa rais wa Jamhuri ya Misri Abd El-fatah El sisi.
Mhandisi Ayman Abd Alwahab mwenyekiti wa kikanda kwa Olimpiki ya walemavu ya kimataifa, Mwenyekiti wa kamati kuu iandaayo michezo, Bwana Charles Nyambi mwenyekiti wa kikanda wa Olimpiki ya walemavu barani Afrika, Msanii Hussen Fahmy Balozi wa Olimpiki ya kimataifa na wanachama wa kamati iandaayo pamoja na idadi ya maafisa wa wizara mbili za vijana na michezo na mshikamano wa kijamii, pia kundi la wachezaji na wajumbe walioshiriki wamehudhuria sherehe ya hitimisho hiyo.
Wakati wa sherehe, wenyeviti wa ujumbe zilizoshiriki katika michezo pamoja na wadhamini wameheshemiwa, pia kuonyesha kwa ripoti iliyosawiriwa kuhusu mashindano muhimu zaidi zilizoshuhudiwa kwa michuano .
Kwa upande wake, Waziri wa vijana na michezo amesifu mashindano mbalimbali ya michezo ambayo michezo ya Kiafrika ya Olimpiki ya walemavu imeyajumuisha, pamoja na uandaaji mzuri, akiashiria uzuri wa utendaji wa wachezaji wakati wa kikao cha michezo, na hii inavutia kujali kwa mataifa ya Kiafrika na wana wake wenye vipawa vya kimichezo kutoka wenye uwezo maalumu.
Dokta Ashraf Sobhy amesisitiza kwamba kujali kukubwa kutoka nchi ya Kimisri kwa watu wenye uwezo maalumu na wanaopinga matatizo na wanahakikisha mafanikio kwa nchi zao katika sekta mbalimbali, kwa uvumilivu wao na uwezo wao juu ya changamoto, akiashiria kuwa mipango na miradi ambayo wizara inaitekeleza kwa watu wenye uwezo maalumu kwa mwaka mzima.
Huku Mhandisi Ayman Abd Alwahab ametoa shukrani na heshima kwa wote waliochangia katika uandaaji wa kikao cha michezo kutoka wanachama wa kamati iandaayo pamoja na vijana wa kujitolea, na hii ili kuhakikisha mafanikio ya michezo na shughuli zake, akisifu zamu muhimu ya wizara ya vijana na michezo na wizara ya mshikamano wa kijamii katika utekelezaji wa kikao cha michezo.
Comments