Waziri wa Vijana na Michezo akutana na wakilishi wa vyama vya wanafunzi katika vyuo vikuu vya kimisri
- 2020-02-02 12:59:51
Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na wakuu kadhaa na wakilishi wa vyama vya wanafunzi katika vyuo vikuu vya kimisri, kwa mahudhurio ya Dokta Ahmed Al-Ansari Gavana wa Fayoum,, Dokta Ahmed Jaber Shedid mkuu wa Chuo Kikuu cha Fayoum, na hii ni pembezoni mwa shughuli za Wiki ya Wasichana katika Chuo Kikuu cha Fayoum kwa toleo lake la tano, inayoandaliwa mnamo Januari 31 hadi Februari 6 ,2020, kwa ushiriki wa wasichana kutoka vyuo vikuu kadhaa vya kimisri.
Waziri wa Vijana na Michezo alisema: "Nafurahi kwa mkutano huu wa vijana na wanafunzi, na tuna shauku katika Wizara ya Vijana na Michezo kwa ya vijana wa chuo kikuu, sambamba na mwelekeo wa uongozi wa kisiasa kwa kuandaa na kuwawezesha vijana. basi Rais El Sisi, tangu kuchukua jukumu la nchi hiyo, ameweka vijana kati ya vipaumbele vyake ,Na mnamo mwaka wa 2016 ulizinduliwa kama mwaka kwa vijana, na kukawa na shauku ya kuwawezesha vijana , na uangalifu wa nchi ndani ya chuo kikuu na wanafunzi wake ukawa mkubwa sana mnamo kipindi hiki "
Kama Dokta Ashraf Sobhy alionyesha shughuli na huduma ambazo wizara hiyo inatoa kwa vijana wote wa Misri bila Utofauti , akieleza kwamba Wizara ya Vijana na Michezo ni nyumba ya vijana wote.
Waziri wa Vijana na Michezo alisikiza mawazo na mapendekezo ya washiriki katika mkutano huo, na alisisitiza kwamba mawazo yote, mipango na mapendekezo ya washiriki yanaheshemiwa, yanathaminiwa na kutekelezwa.
Inataja kuwa Jumamosi mchana, Waziri wa Vijana na Michezo na Waziri wa Mazingira walikuwa wamefungua awamu ya kwanza ya mradi wa Baiskeli ya kugawana “bike sharing”, unaotekelezwa chini ya kauli mbiu "Baiskeli ni njia ya usafirishaji" kwenye Chuo Kikuu cha Fayoum.
Comments