Madbuly: Misri ina matarajio ya kukaribisha makao makuu ya kiutendaji ya Sekretarieti ya mkataba wa biashara huru wa kiafrika..... na serikali inatoa usaidizi wote wa uwezekano kwa jambo hilo.
Waziri mkuu anasisitiza juu ya umuhimu wa mkataba wa biashara huru wa kiafrika kwa athari zake chanya zitakazopatikana katika kuimarisha ushirikiano na ukamilifu katika nchi za bara.
Leo Dokta Mustafa Madbuly"Waziri mkuu" alipokea ujumbe wa kameshina ya Umoja wa kiafrika unaozuru Misri, na mkutano huo ulihudhuriwa na Mhandisi Amr Nassar"Waziri wa biashara na viwanda", na Balozi Khaled Ammar "Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje".
Na Mshauri Nader Saad "Msemaji rasmi wa urais wa baraza la mawaziri" alisema : Ziara hii ya ujumbe wa Kameshina ya Umoja wa kiafrika inafanyika kwa ajili ya kutathmini faili ya kukaribisha Misri kwa makao makuu ya kiutendaji ya mkataba wa biashara huru wa kiafrika, nao ni mkataba unaolenga kuongeza ukubwa wa utegemezi wa nchi wanachama na kuimarisha uwezo wa kushindana kwa kutengeneza barani Afrika, akiashiria kwamba hii itafanyikwa kupitia kuondoa vikwazo vya Forodha au visivyo hatua kwa hatua, vinavyokwamiza shughuli za biashara.
Na mnamo mkutano Waziri mkuu alisisitiza juu ya umuhimu wa mkataba wa biashara huru wa kiafrika, na athari zake zitakazopatikana katika kuimarisha ushirikiano na ukamilifu Kati ya nchi za bara, akiongeza kwamba Rais Elsisi anatilia mkazo kwa kuutekleza mkataba huu Kama kipengele kimoja cha vipengele vya urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika.
Na Dokta Mustafa Madbuly aliashiria kwamba Misri inazingatiwa miongoni mwa nchi za kwanza zilizotia saini mkataba huu, na mnamo siku fulani inayotarajiwa kuingiza mkataba huu kwa uteklezaji, baada ya kuamini kwa mkataba huu toka nchi 22 hadi sasa.
Madbuly alisema kwamba :Misri inathamini umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za bara khasa katika uwanja wa biashara, kulingana na kuondoa vikwazo vya Forodha kutachangia kupunguza bei za bidhaa, pia kuhudumia malengo ya kuhakikisha maendeleo endelevu barani Afrika.
Pia Waziri mkuu alisisitiza juu ya kwamba Misri inatarajia kukaribisha makao makuu ya kiutendaji ya Sekretarieti ya mkataba wa biashara huru wa kiafrika, na serikali inatoa usaidizi wote wa uwezekano kwa jambo hilo, aliashiria kwa miundombinu ya kimaendeleo, na uwezo mkubwa wa vifaa na vyombo yatakayowezesha Misri kuwa na makao makuu bora kwa Sekretarieti ya mkataba.
Na kutoka upande wao, wanachama wa ujumbe wa kameshina ya Umoja wa kiafrika walieleza Furaha yao ya kuitembelea Misri kwa ajili ya kutathmini faili ya kukaribisha makao makuu ya kiutendaji ya mkataba wa biashara huru wa kiafrika, wakisisitiza kwamba watatathmini faili za nchi zilizoomba kukaribisha makao makuu, kulingana na Maoni yao na maandalizi katika nchi zilizochaguliwa, pia walisifu usaidizi unaotolewa kwa Misri kwa Uongozi wa Rais Elsisi "Rais wa Umoja wa kiafrika "kwa masuala ya ushirikiano na maendeleo barani Afrika, na juu yao eneo la biashara huru ya kiafrika.
Comments