Bingwa Fatma Omar anaendelea mafanikio yake kwa medali mpya katika kombe la dunia la Paralympiki

Bingwa Fatma Omar anaendelea mafanikio yake ya kibinafsi baada ya kuhakikisha medali ya kifedha katika michuano ya kombe la dunia la Paralympiki inayofanyika nchini Nigeria, kwa uzito 67+, kwa kuinua uzito wa kilogramu 121.


Bingwa Fatma Omar  mchezaji wa kwanza katika historia ya Misri, Afrika na Waarabu anayehakikisha medali 5 katika vikao vitano vya Olimpiki mfululizo, kuanzia Sydney 2000, hadi Rio 2016, medali 4 ni za kidhahabu mfululizo.

Ameteuliwa mara nyingi kama mchezaji bora zaidi katika orodha za kamati ya kimataifa ya Paralympiki mnamo mwaka wa 2012, mwenye rekodi  ya kimataifa katika uzito wa kilogramu 56, na ameinua uzito wa kilogramu 142, na amevunja rekodi ya dunia na ya Olimpiki na ilisajiliwa kwa jina lake.


Fatma Omar   anazingatiwa bingwa wa kuinua  uzito sio kwenye ngazi ya kiarabu na Kiafrika tu, bali ulimwenguni.


Kwa upande wake, Fatma Omar anazingatia kuwa medali mpya anayeihakikisha ni hatua kwenye kurudi kwake nguvu kwa mashindano, baada ya kipindi ambapo amekuwa akiugua jeraha wakati huo na kutozoeza, ila chache, akisisitiza kuwa kipindi kijacho kitakuwa kizuri pamoja na ahadi ya kufanya juhudi kubwa zaidi ili kuhakikisha matumaini yaliyowekwa juu yake kwa kushinda medali mpya katika Olimpiki ya Tokyo mnamo majira ya joto 2020.

Comments