Kairo inapokea kundi la nyota wa Tenisi baada ya "Australia wazi"

Kairo mnamo Alhamisi ilipokea wachezaji wa Tenisi  wa kike wanaoshiriki katika mashindano ya "Z wazi ya  Kimataifa kwa Wanawake " yaliyopangwa kufanyika Februari 10,  yatakayoendelea hadi Februari 16, huko Sheikh Zayed.


Mabingwa 64 wa Tenisi  wa mashindano ulimwenguni wanashiriki katika ratiba ya mashindano ya kimsingi, kwa kuongeza wanawake 18 kutoka wahitimu wa raundi ya 64 kwa majukumu makuu katika mashindano hayo mnamo Februari 9, 2020.


Mashindano hayo ni moja wapo ya mashindano makubwa ya kimataifa kwa wanawake  ulimwenguni na ni ya kwanza ya aina yake huko Kairo ,  inayojumuisha wachezaji wengi wa kimataifa waliowekwa katika ainisho la Shirikisho la Tenisi  la kimataifa, pamoja na Kazakhstan Zarina Diaz walioshika nafasi ya 73 ulimwenguni,  inayoongeza orodha ya kiuumla ya mashindano  Mholanzi Arancha Ross alishika nafasi ya 93 ulimwenguni, na Lesia Tsurenko wa Ukranie,  aliyekuwa na nafasi nzuri zaidi katika 23 ulimwenguni mwaka wa 2019 kabla ya kujeruhiwa na kuanguka kwenye nafasi ya 128,  na mashindano yale ni nafasi nzuri kwake kupata tena nafasi yake na kurudi kwenye mashindano.


Mashindano hayo yanashuhudia ushiriki bora wa wachezaji wa Misri, Mayar Sharif, aliyekuwa na  nafasi ya 188 ulimwenguni, na mashindano hodari kwa taji la mashindano hayo, ambayo yamepangwa kushindana katika Olimpiki ya Tokyo 2020, pamoja na nyota maaarufu Sandra Samir, aliyeorodheshwa namba 367 ulimwenguni.

Comments