Wizara ya vijana na michezo "ofisi ya vijana waafrika -idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia" inatoa matukio ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika, k kushirikiana na mashirikisho na taasisi kadhaa za kitaifa, na hayo mnamo kipindi cha 8 hadi 22 Juni ijayo kwenye kituo cha Elimu ya kiraia katika kituo cha vijana wa AlJazira Mjini Kairo.
Udhamini unalenga kuhamisha Jaribio kale la kimisri la kujenga taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha viongozi vijana waafrika wenye mitazamo yanayosawazisha na mielekeo ya urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika, mielekeo yenye imani ya kuhudumia malengo ya umoja wa kiafrika kupitia Ukamilifu, pamoja na kuunda mkusanyiko wa viongozi vijana waafrika wenye athari kubwa barani kupitia mafunzo, uzoefu unaohitajika, na mitazamo ya kimikakati.
Udhamini unawalenga viongozi watendaji 100 kutoka nchi wanachama za Umoja wa kiafrika, wenye maamuzi katika sekta ya kiserikali, viongozi watendaji katika sekta binafsi, vijana wa jamii ya kiraia, wakuu wa mabaraza ya kitaifa kwa vijana, waatalamu wa vyuo vikuu, watafiti katika vituo vya tafiti za kimikakati na kimawazo, wanachama wa vyama vya kiufundi, na waandishi wa vyombo vya habari.
Udhamini wa Nasser unazingatiwa mmoja wa vyombo vya uteklezaji wa mpango wa( Milioni moja kwa kufikia 2021) ili kuwawezesha vijana milioni moja kwa kufikia mwaka wa 2021, mpango uliotolewa kwa Kameshina ya Sayansi, Teknolojia, na Rasilimali za binadamu katika Umoja wa kiafrika mwezini Aprili 2019. Pia Udhamini unazingatiwa mmoja wa vyombo vya " kutumia marudio ya kidemografia(idadi ya watu) kupitia kuwawekeza vijana , na hayo ni sawa sawa na utawala wa Misri wa Umoja wa kiafrika 2019.
Udhamini wa Nasser unazingatiwa udhamini wa kwanza wa (Kiafrika kiafrika) unaolenga viongozi vijana waafrika wenye vitengo tofauti vya uteklezaji ndani ya jamii zao, nao ni mmoja wa vipengele vikali vya kuwezesha kwa ugeuzi wa kiafrika vilivyotolewa kwa Ajenda ya Afrika 2063,na hayo ili kusisimua na kuimarisha maadili ya kiafrika kupitia kujitegemea, ushikamano, kazi kwa bidii, ustawi wa ujumla, na kujenga juu ya mafanikio ya kiafrika, uzoefu, na harakati nzuri zaidi ili kuunda mfumo wa kiafrika kwa mabadiliko na maendeleo.
Na hayo yote yanakuja kulingana na shime ya Wizara ya vijana na michezo juu ya kuimarisha mchango wa vijana waafrika kupitia kutoa njia zote za usaidizi, uwezeshaji, na utoaji mafunzo, pamoja na kuwawezesha kwenye vyeo vya Uongozi na kupata faida toka uwezo na mawazo yao, kwa kutekleza yaliyotangazwa na Rais Abd Elfatah Elsisi-Rais wa Jamhuri mnamo matukio ya mkutano wa vijana wa dunia, ulioshuhudia uwakilishi adhimu kwa vijana wa nchi za kiafrika, pia kwa kutekleza uamuzi wa Rais kwa 2019 uwe mwaka wa Elimu.
Inatajwa kwamba Taasisi kuu kwa Maarifa kupitia tovuti ya kielektroniki iliyotolewa kwa mnasaba wa urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika inatoa maelezo na taarifa za Udhamini kwa tovuti nane kwenye mitandao ya intaneti kwa lugha hizi: Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, kiswahili, kihausa, kiamhari, kireno, na kichina.
Na Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kimageuzi" ulishuhudhia ujio mkubwa wa vijana wa nchi za kiafrika mnamo siku za kusajili, amabpo idadi ya waliotangulia ilifikia viongozi vijana 851 wanaowakilisha nchi 51 za kiafrika toka vitengo tofauti.
Comments