Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote anaesema katika Qurani tukufu:
{إِنَّ هَذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا}
Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa.
Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye pekee asiye na mshirika wake na ninashuhudia ya kwamba Bwana Wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila mwenye kuwafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Na baada ya Utangulizi huu:
Ndugu zangu Waislamu, hakika pande mbalimbali za Utukufu wa Qurani tukufu hazina kikomo cha idadi na hazihesabiki. Qurani tukufu ni kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, isiyokatika, na ni ukumbusho wenye hekima, na ni Nuru iangazayo na ni Njia iliyonyooka ambayo haijongelewi na upotoshaji na wala haifikiwi na kilichobadilika kwa upande wowote na wala Wanachuoni hawatosheki nayo, wala haichoshwi na wingi wa kujibu, na maajabu yake hayamaliziki, atakayesema kwa kuitumia Qurani atakuwa msema kweli, na atakayeifanyia kazi Qurani atalipwa, na atakayehukumu kwa Qurani atakuwa mwadilifu, na atakayeilingania ataongozwa katika Njia iliyonyooka. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَى لِلْمُسْلِمِينَ}
Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{مَا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِنْ شَيْءٍ}
Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa.
Na katika pande mbalimbali za Utukufu wa Qurani tukufu ni utunzaji wake wa Ujenzi wa Kimaadili katika Maisha ya kila mtu na ya Mataifa kupitia Mfumo wa Maadili na Misingi na Mizizi iliyopangika ya mienendo ya Kiutu ambayo inaiasisi Jamii iliyofungamana yenye nafsi zilizo safi na nyoyo zilizotakata, wenyewe wanatangamana na kushirikiana wao kwa wao kwa ukweli, Uaminifu, Kuhurumiana, na Uadilifu, na kila mmoja wao anamwamini mwenzake kwa Sunna ya Watu Kuhitilafiana kibinadamu, kuishi kwa amani, kumheshimu mwingine na kuhangaikia ujenzi wa Dunia kwa Dini, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ}
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ * إِلَّا مَنْ رَحِمَ رَبُّكَ...}
Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana,
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{هُوَ أَنْشَأَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا}
Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo.
Na Mzingativu wa Aya za Quran tukufu anatambua kwa yakini kwamba Maadili mazuri ya Kitabia yanayolinganiwa na Qurani tukufu sio aina moja katika aina nyingi za burudani ambayo inaweza kuachwa, au kuifanyia kazi katika mazingira fulani pasi na mengine, bali ni mkusanyiko wa Maadili yenye thamani ya Kitabia yaliyo thabiti ambayo hayabadiliki kwa kubadilika zama na hayawi tofauti kwa tofauti ya sehemu, na hakuna dalili nzuri zaidi kuliko ile ya kwamba Maadili haya ya Kitabia yalikuwa mfumo wa Maisha alioufanyia kazi Mtume S.A.W, na akauhimiza na kuulingania. Na Mama wa Waumini, Bi Aisha R.A, alipoulizwa kuhusu Tabia za Mtume wetu S.A.W, hakumjibu muulizaji kwa sentensi yenye mkusanyiko wa aina mbalimbali za Tabia, bali jibu lake lilikuwa Qurani tukufu, kutoka kwa Saad bin Hisham, katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَإِنَّكَ لَعَلَى خُلُقٍ عَظِيمٍ}
Na hakika wewe una tabia tukufu.
Amesema: Nilimuuliza Bi Aisha R.A, nikasema: Ewe Mama wa Waumini, ninaomba unielewe Tabia za Mtume S.A.W. Akasema: Hakika ya Tabia za Mtume S.A.W, zilikuwa Qurani tukufu.
Na katika maelekezo ya Bi Aisha R.A, kwa muulizaji wake kuna hakikisho la kuwa Qurani yote ikiwemo Akida zote, Sheria na Ibada, vyote hivyo kimsingi ni wito wenye nguvu wa kumjenga Mtu Kitabia na kwa ukamilifu. Na Mtume S.A.W, alikuwa ruwaza njema ya Ujenzi huu katika Mambo yote yanayoyahusu Maisha yake.
Na miongoni mwa Maadili Mema yaliyo Muhimu ni: Ni kuuheshimu Utu wa Mtu na kuilinda heshima yake na kutomdharau. Na hii ni Amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyomo katika kitabu chake kitukufu kwa ajili ya muumini, ili Muumini huyu aweze kuiepusha nafsi yake na kila kinachoziudhi hisia za Watu, kama vile dharau na Utani, na dhana mbaya.
Na miongoni mwa Maadili Mema ni kuuheshimu Utu wa Mtu, na kuiheshimu heshima yake na kutomdharau na kumpuuza. Na hii ni Amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyomo Msahafuni kwa waumini Wote kwamba kila mmoja ajiepushe na kila kitu kinachoweza kuwaudhi wengine kihisia, kama vile dharau na Utani, na kuwadhania vibaya. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَى أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَى أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ}
Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ}
Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.
Qurani tukufu inaamrisha usafi wa moyo na kusalimia mtu na kila aina ya Mambo mabaya na chuki, na kutomdhania mtu yoyote ubaya. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{لَّوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا هَذَا إِفْكٌ مُّبِينٌ}
Kwa nini mlipo sikia khabari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhaahiri?
Na katika Maadili ambayo Qurani tukufu imeyapa umuhimu wa kuimarisha mizizi yake ni: Maadili ya Ushirikiano, Kupeana, na Kuhurumiana. Qurani tukufu imeiamrisha Jamii kwa matabaka yake yote, iwe na Ushirikiano kwa Wema na Uchamungu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ}
Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
Kwa hiyo, Ushirikiano baina ya Watu, ni moja kati ya elementi za Nchi kuwa na nguvu, na kuleta Usalama wa Kijamii kwa wananchi wake. Kila mtu ana mahitaji yake anayoyahangaikia ili ayapate. Na anajitahidi kuyafikia. Na Moyo wa kuleana unapoongezeka katika Jamii, basi Jamii hiyo hutulizana katika kuyaelekeza mahitaji hayo, bali huharakisha katika kunyanyua thamani ya Kuleana katika Jamii kwa Kiwango cha juhudi na nguvu zake.
Anasema Mshairi:
Watu wao kwa wao, wawe waarabu au waajemi
wanatumikiana na hata kama hawahisi hivyo.
Mtume S.A.W, ameelekeza thamani ya Kushirikiana katika Hadithi nyingi, ambapo anasema: Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, Kuhurumiana kwao na kuoneana upole, ni kama mwili mmoja, ambapo kiungo kimoja kinapojisikia maumivu basi mwili mzima huugulia kwa kukesha na homa kali.
Na anasema Mtume wetu S.A.W: Muislamu Ndugu yake ni Mwislamu mwenzie, hamdhulumu, na hamwachi adhuriwe. Na yoyote atakaye msaidizi nduguye Mwislamu katika haja yake, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamsaidia yeye katika haja yake. Na atakayemwondoshea tatizo, Mwenyezi Mungu Mtukufu atamwondoshea tatizo katika matatizo Siku ya Kiama. Na atakayemsitiri Mwislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu atamsitiri siku ya Kiama.
Na miongoni mwa Maadili yenye thamani kubwa ni Thamani ya Kufikiri na kuitumia Akili. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamrisha Waja wake kufikiri uumbwaji wa Mbingu na Ardhi, na akawasifu wenye kufikiri, akasema S.W:
{إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِأُولِي الْأَلْبَابِ * الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَى جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ}
Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{أَوَلَمْ يَنْظُرُواْ فِي مَلَكُوتِ السَّمَاوَاتِ والأَرْضِ}
Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi…
Na ametufungulia sisi milango ya kuzingatia na kufikiria, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{اللَّهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا}
Mwenyezi Mungu aliye ziinua mbingu bila ya nguzo mnazo ziona…
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{ قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ جَعَلَ اللَّهُ عَلَيْكُمُ النَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَهٌ غَيْرُ اللَّهِ يَأْتِيكُمْ بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ فِيهِ أَفَلَا تُبْصِرُونَ}
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya mchana umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni usiku mkapumzika humo? Basi je, hamwoni?
Vilevile Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha kufikiri katika Nafsi, akasema:
{أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُواْ في أَنفُسِهِمْ}
Je! Hawajifikirii nafsi zao?
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِلْمُوقِنِينَ * وَفِي أَنْفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ}
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?
Kwa hiyo, Quran tukufu inatufungulia mlango wa kufikiri katika kila kinachomnufaisha mwanadamu, na kufikiri huko ni ibada ambayo Maswahaba wa Mtume S.A.W, radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziwafikie Wote, waliijua vilivyo na wakalitambulia lengo lake. Anasema Abu Dardaau R.A: hairefuki fikra ya Muumini kamwe isipokuwa huwa ameifahamu, na huwa hafahamu isipokuwa atakuwa anajua, na haelewi isipokuwa atakuwa ameifanyia kazi.
Na miongoni mwa Maadili Mema ni: Maadili ya kuzungumza, na kuwaheshimu Wengine. Aya nyingi za Qurani tukufu zinauongoza Uma, bali zinauongoza Utu Wote kuelekea katika umuhimu wa mazungumzo katika Maisha ya Watu. Mazungumzo ni njia aliyoiridhia Mwenyezi Mungu Mtukufu kama Mfumo wa Mitume katika kufikisha ujumbe wake kwa Watu; na huo ndio Uislamu unaoamini Uhuru wa Itikadi. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ قَدْ تَبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ}
Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu.
Tunamwona Mtume Nuhu A.S, akizungumza na Watu wake katika hali miongoni mwa hali mbalimbali za Maisha yake Marefu ya Kulingania, anasema:
{..يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِنْ كُنْتُ عَلَى بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّي وَآتَانِي رَحْمَةً مِنْ عِنْدِهِ فَعُمِّيَتْ عَلَيْكُمْ أَنُلْزِمُكُمُوهَا وَأَنْتُمْ لَهَا كَارِهُونَ} .
Enyi watu mnanionaje kama nitakuwa katika ubainifu kutoka kwa Mola Wangu Mlezi, imenijia rehma kutoka kwake na ukafunikwa kwenu
Huyu ni Mtume wetu Ibrahim A.S, akitoa hoja kwa Mfalme Maliepotoka, katika mazungumzo ya kiakili ambayo Quran tukufu inatutengenezea picha hiyo kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِي حَاجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ أَنْ آتَاهُ اللَّهُ الْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ قَالَ إِبْرَاهِيمُ فَإِنَّ اللَّهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ فَبُهِتَ الَّذِي كَفَرَ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ}
Hukumwona yule aliye hojiana na Ibrahim juu ya Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim alipo sema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuisha na kufisha. Ibrahim akasema: Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
Na kwa Mfumo huo huo, Mtume Wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mtume Muda A.S, aliufuata katika mazungumzo yake na Firauni, na katika hili, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ * قَالَ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِنْ كُنْتُمْ مُوقِنِينَ * قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُ أَلَا تَسْتَمِعُونَ* قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ * قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ الَّذِي أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ * قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ * قَالَ لَئِنِ اتَّخَذْتَ إِلَهًا غَيْرِي لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ الْمَسْجُونِينَ}
Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote? Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini. (Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi? (Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza. (Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu. (Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini. (Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani.
Hakika Quran tukufu katika kuweka misingi imara ya Thamani ya Mazungumzo, ni wito wa kumea kwa Utu, na kumuheshimu mwingine bila ya kujali rangi, dini au jinsia yake, na kuupiga vita mtazamo wa upande mmoja na wa kibaguzi na kujikweza, ambapo Quran tukufu inamlindia Mwanadamu Utukufu wake kwa ajili ya Utu na sio kwa ajili ya kitu kingine chochote. Na imeikiri asili yake moja bila kujali tofauti zozote za Watu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى كَثِيرٍ مِمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا}
Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالا كَثِيرًا وَنِسَاءً وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالأرْحَامَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا}
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni
Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na akusameheni Nyinyi.
أ
* * *
Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye pekee asiye na mshirika wake na ninashuhudia ya kwamba Bwana Wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila mwenye kuwafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Ndugu zangu Katika Uislamu:
Miongoni mwa Maadili yenye thamani kubwa Kimaadili ambayo Quran tukufu inayolingana ni: Kuidhibiti Nafsi na kuzuia Hasira. Inajulikana kwamba Mwanadamu katika Maisha haya hasalimiki na kukumbana na baadhi ya hali au matukio ambayo yanaweza kumkasirisha na kuchochea hasira zake; Na nafsi ya mtu inaguswa na kuathirika kwa yale inayoyasikia na inayoyaona. Na kuna maandiko mengi yamekuja katika Quran tukufu ambayo yanalingania kuidhibiti nafsi na kuzuia Hasira, na yanalingania mwenendo wa kupeana mikono kama ni njia ya kusameheana. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَسَارِعُوا إِلَى مَغْفِرَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ الَّذِينَ يُنْفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ}
Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu. Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنْكُمْ وَالسَّعَةِ أَنْ يُؤْتُوا أُولِي الْقُرْبَى وَالْمَسَاكِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا أَلَا تُحِبُّونَ أَنْ يَغْفِرَ اللَّهُ لَكُمْ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ}
Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَلا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلا السَّيِّئَةُ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ وَمَا يُلَقَّاهَا إِلاَّ الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلاَّ ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ}
Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ}
Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu.
Na katika Maadili yenye thamani: ni kuwasuluhisha Watu waliogombana. Wingi ulioje wa aya za Quran tukufu zinazolingania na kuwaamrisha kuwapatanisha Watu! Na zinawabashiria wenye kuwapatanisha watu, kwamba wana wao malipo makubwa mno. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{لاَ خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِنْ نَجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلاَحٍ بَيْنَ النَّاسِ وَمَنْ يَفْعَلْ ذَلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاةِ اللَّهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا}
Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{فَمَنْ خَافَ مِنْ مُوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ}
Na mwenye kumkhofia muusiaji kwenda kombo au kupata dhambi akasuluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ اليَتَامَى، قُلْ إِصْلاَحٌ لَهُمْ خَيْرٌ، وَإِنْ تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ المُفْسِدَ مِنَ المُصْلِحِ، وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَأَعْنَتَكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ}
Na wanakuuliza juu ya mayatima. Sema: Kuwatengenezea ndio kheri. Na mkichanganyika nao basi ni ndugu zenu; na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji. Na Mwenyezi Mungu angeli penda angeli kutieni katika udhia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hekima.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anaesema Kweli, ametoa onyo kali kwa wenye kuvuruga baina ya Watu, akasema:
{وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللهَ عَلَى مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ * وَإِذَا تَوَلَّى سَعَى فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ وَاللهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ * وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ}
Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ugomvi. Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.
Ni kwa kiasi gani sisi tuna haja ya kushikamana na Maadili yenye thamani ya Kitabia yaliyolinganiwa na Uislamu katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mtume wetu S.A.W, akayatekeleza, mpaka tufikie Kiwanga cha Ustaarabu na Maendeleo na Ustawi, walichokifikia Mababu zetu. Anasema Msemaji mwenye Hekima:
Hakika ya Mataifa yaliendelea kuwepo kwa Tabia zao njema.
Na zilipowatoweka Tabia zao njema na wao pia walitoweka.
Ewe Mola Mlezi tunakuomba utuongoze tuzifikie Tabia zilizo njema zaidi, na hakuna wa kutuongoza kuelekea katika Tabia zilizo njema zaidi isipokuwa wewe, tunakuomba utuepushe na Tabia mbaya vna hakuna wa kutuepusha isipokuwa wewe. Tunakuomba uzilinde Nchi zetu na wananchi wake, na Majeshi yake ya Ulinzi na ya Usalama, na uturuzuku Usalama na Amani, sisi na Nchi zote Duniani.
Comments