Medali 15 kwa Misri katika siku ya tatu ya michuano ya Afrika kwa Karate

 Timu ya kitaifa ya Misri kwa Karate imeshinda medali 15, medali 3 za kidhahabu, medali 8 za kifedha na medali 4 za shaba katika siku ya tatu ya michuano ya Afrika kwa Karate inayofanyika nchini Morocco mnamo kipindi cha tarehe 7 hadi 9 Februari.

 

Wachezaji walioshinda medali za kidhahabu ni : Giana Farouk (uzito wa kilogramu 61 wasichana), Feryal Ashraf (uzito wa kilogramu 68) na Abdallah Mamdouh (uzito wa kilogramu 75 wanaume).

 

Wanaoshinda medali za kifedha ni : Sara Essam katika kata wasichana, Ahmed Ashraf katika kata wanaume, Radwa Sayed (uzito wa kilogramu 50 wasichana), Ali Alsawy (uzito wa kilogramu 67 wanaume), TaHa Tarek (uzito wa kilogramu 84+ wanaume) na Mohamed Ramadhan (uzito wa kilogramu 84 wanaume) na kata ya pamoja wasichana, komete ya pamoja wanaume.

 

Walioshinda medali za shaba ni : Malek Gomaa (uzito wa kilogramu 60 wanaume), Yasmin Hamdy (uzito wa kilogramu 55 wasichana), Shaimaa Abo Alyazeed (uzito wa kilogramu 68) na kata ya pamoja wanaume.

Comments