chini ya uangalifu wa Rais Abdel Fattah El-Sisi .. Sheikh Al-Azhar na Waziri wa Uhamiaji wazindua mpango wa "Misri mwanzo wa njia"

Balozi Nabila Makram: Mpango huo utajumuisha viongozi wote wa juu na mawaziri kutoka nchi nyingine ambao wamepokea elimu yao nchini Misri

 

Dokta . Ahmed El-Tayeb:  baadhi ya Wahitimu wa Al-azhar wamepata nafasi za juu katika nchi zao na wamechangia sana maendeleo zao .

 

mheshimiwa Imamu Mkuu dokta. Ahmed Al-Tayeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif  amepokea  Balozi Nabila Makram Abdul-Shahid, Waziri wa Nchi kwa Uhamiaji na Mambo ya wamisri nje ya nchi, kujadili mpango unaoitwa "Misri mwanzo wa njia."

Mwanzoni mwa mkutano, Balozi Nabila Makram alielezea kuwa mpango huo "Misri ni mwanzo wa njia" wakati wake sherehe itaandaliwa ili kuwaalika viongozi wote wakuu na mawaziri kutoka nchi za Kiafrika na nchi za Kiarabu pamoja na wahitimu wa nchi za Asia ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar na vyuo vikuu vya kimisri. akielezea alionyesha mpango kwa Mheshemiwa rais Abd El fatah Elsisi , na  sherehe hii itaheshemiwa kwa uangalifu wake,  na Mheshemiwa Rais pia alielekea pamoja na ushirikiano na Al-Azhar Al-Sharif, Wizara ya Elimu ya Juu na vyuo vikuu vya kimisri ili kuiandaa.

Balozi Nabila Makram aliongeza kuwa sherehe hiyo inakuja katika mfumo wa kusisitiza jukumu la kuongoza kwa hali ya Misri juu ya pande za Kiafrika na Kiarabu na kuimarisha uhusiano na nchi za Asia.Ni pia inakuja katika mfumo wa tangazo la Rais la kufanyika 2019  mwaka wa elimu   na kwa kushirikiana na urais wa Misri wa Umoja wa kiafrika.

Balozi Nabila Makram alisema kuwa wahitimu wageni  wa al-Azhar ni chanzo kuu cha nguvu muhimu sana za Misri ulimwenguni, akielezea kuwa utawala wa  baadhi ya wahitimu wa al-Azhar walikuwa na nafasi za juu katika nchi zao, unasisitiza nguvu za Al-Azhar na athari zake duniani. Akifafanua kuwa mnamo programu ya sherehe kila mgeni mhitimu atatoa hotuba inayoelezea kitivo ambapo alihitimu.

Kwa upande wake, Imamu wa Al-Azhar Alisema Al-azhar  kila mwaka inapokea wanafunzi kutoka nchi zaidi ya mia moja, na hutoa msaada kamili kwa wanafunzi hawa, wakipokea elimu za kidini na kidunia na kisha hurudia nchi zao  kama mabalozi wa Uislamu na Amani, akielezea kuwa baadhi ya wahitimu wageni wa Al-Azhar wamekuwa na nafasi za juu Katika nchi zao, na kuchangia sana kwa maendeleo na utamaduni  wa nchi zao, na kufanya kazi ili kukuza maadili ya Usamehe na kuwepo kwa ushirikiano waliyojifunza huko Al-Azhar.

 

Mwishoni mwa mkutano huo, ilikubaliwa kuunda timu ya  kazi kutoka Al-Azhar Al-Sharif na Wizara ya Uhamiaji, ili kuratibu kati yao wenyewe kujiandaa kwa ajili ya sherehe.

برعاية الرئيس السيس

Comments