Hana Goda anashiriki pamoja na timu ya wanawake Katika mashindano ya ulimwengu kwa Tenisi ya meza
- 2020-02-12 19:36:36
Wafanyikazi wa kiufundi wa timu ya wanawake kwa Tenisi ya meza, iliyoongozwa na Ashraf Helmy, waliamua kumjumuisha Hana Goda, mchezaji mdogo chini ya miaka 12, ili kushiriki na wanawake katika mashindano ya ubingwa wa dunia yatakayofanyika kutoka Machi 22 hadi 29 nchini Korea Kusini.
Msichana Hana ameshinda mashindano mengi na majina yake , ya mwisho ambayo huchapishwa na Uainishaji wa Kimataifa wa Vijana Wanawake Ulimwenguni mwote, kulingana na Shirikisho la Kimataifa.
Alishinda pia medali ya kidhahabu ya Mashindano ya Kimataifa ya Ureno katika Mashindano ya vijaan chini ya miaka 12 na 15, na shaba ya Mashindano ya dunia wka mabara, katika mafanikio ambayo hayakuwahi kutekelezwa katika historia ya tenisi ya meza ya kimisri.
Wachezaji wa tenisi wa kiume na wa kike walifanikiwa kufikia nafasi za juu katika mashindano ya ubingwa wa Kimataifa wa Ujerumani, ambayo ni moja ya safu kubwa ya ubingwa wa Shirikisho la Kimataifa.
Omar Asr alifikisha nafasi ya tatu katika mashindano ya umoja kwa wanaume, baada ya kumshinda mchezaji huyo wa Korea Kusini, ambapo alifanikiwa kubadilisha matokeo kutoka kushindwa kwa 3/1 hadi ushindi wa 4/3, na Ahmed Saleh pia alifikia nafasi ya tatu baada ya kumshinda mchezaji wa Austria mwenye mizizi ya Uchina kwa 4/1, Khaled Asr alijiunga nao katika raundi hiyo hiyo baada ya busara na ushindi wake dhidi ya mchezaji wa Kibulgaria 4/0, na vile vile mchezaji wa Argentina kwa tija sawa.
Katika shindano la umoja kwa wanawake, Yousra Helmy alifikia raundi ya tatu baada ya kumshinda mchezaji wa Hungary kwa 4-0, Dina Musharraf akishindana na mashindano, na katika mashindano yaliyokuwa yakichanganywa mara mbili, wawili wamisri Omar Asr na Dina Musharraf walishinda wawili wapolanda kwa 3/0 na kufikia kwao raundi ya pili.
Comments