Mona Ahmed (Binti wa Aswan), mhitimu wa kundi la kwanza kutoka Shule ya kiafrika 2063, anashindana katika mashindano ya "Mkono wako pamoja na sisi (Eidak Maana) "
- 2020-02-13 10:51:52
Wizara ya Vijana na Michezo ilizindua mashindano ya "Mkono wako pamoja na sisi(Eidak Maana) " ya kusaidia juhudi za vijana na kuangazia viongozi wa vijana wa eneo hilo wanakuwa na uwezo wa kushikilia miradi na kupatikana nafasi kwako kwa kufanikisha hatua zao za maendeleo, na Mona Ahmed anashindana katika mashindano hilo kupitia mpango wa "(Wazo na Kisa)", aliyeuanzisha kwa ajili ya kueneza uelewa wa watoto na vijana kwa kiutambulisho na utamaduni wa kiafrika.
Mona alianza harakati hiyo baada ya kuhitimu kutoka kwa kundi la kwanza la Shule ya Majira ya Kiafrika 2063 mwaka mmoja uliopita, na mnamo kipindi hicho alifanikia kuwahitimu makocha wachanga wanne wenye umri wa kuanzia miaka 11 hadi 15 (Abd ElRahman, Abd El Rahman, Israa na Basmala), na waliweza kufanya semina juu ya tamaduni za Kiafrika , linalozingatia mfano wa kweli wa dhana ya mwendelezo, uendelevu na upanuzi wa jukumu la Shule ya Kiafrika katika kufanikisha dhana ya uendelevu kikamilifu.
Kwa msingi, Mona anajitahidi kupitia mpango wake, kufanya semina za kielimu, hadithi kutoka fasihi ya Kiafrika, hadithi za sanaa za jadi na vigano vya Kiafrika, pamoja na uhusiano wa pamoja wa kitamaduni na kihistoria, harakati za ukombozi wa kitaifa na baba waanzishi wa Umoja wa Afrika, na hayo yatafanyika mashuleni, majumba ya kitamaduni na vituo vya vijana ndani ya mkoa wa Aswan, na mnamo Machi 2019, alikaribishwa na "Idara ya Utafiti wa kisayansi" kwenye athari za Aswan na Nubia kwa kushirikiana na Kitivo cha Mambo ya kale katika semina ya elimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kama moja wapo ya mifano ya vijana bora, kama ilivyokuwa akishikiliwa na Kitivo cha Biashara, Chuo Kikuu cha Aswan mnamo Novemba 2019, kama msemaji juu ya mpango huo, jukumu lake na kwa Hati ya Vijana wa Kiafrika.
Mona hufanya kama Nguvu zenye nyoro inayosaidia mitazamo ya nchi ya kimisri, na lengo lake ni kuandaa kizazi kinachoamini katika umoja wa Kiafrika na msingi wa Kiafrika kama moja ya matarajio ya Ajenda 2063.
Comments