Misri imeshinda medali 8 wakati wa kushiriki kwake katika michuano ya Afrika kwa watu wazima kwa mpira wa vinyoya inayofanyika kwenye sebule namba 2 katika uwanja wa kimataifa wa Kairo mnamo kipindi cha tarehe 10 hadi 16, mwezi huu wa Februari.
Medali za mafarao ni :
Medali 3 za kidhahabu kupitia
medali ya kidhahabu kwa wanawake wawili ambao ni Hadia Hosny na Doha Hany,
medali ya kidhahabu kwa watu wawili Adham Hatem na Doha Hany pamoja na medali
ya kidhahabu ya timu ya wanawake.
Pia timu ya kitaifa ya Misri
imepatia medali 5 za shaba ambazo ni : medali ya shaba ya kibinafsi ya wanaume
kupitia Adham Algamal, medali mbili za shaba za kibinafsi za wanawake kupitia
Hadia Hosny na Doha Hany, pamoja na medali ya shaba kwa watu wawili ambao ni
Ahmed Salah na Hadia Hosny, mwishoni medali ya shaba kwa timu ya wanaume.
Sherehe za kupokea medali
imehudhuriwa na mwenyekiti wa shirikisho la Kiafrika la mpira wa vinyoya (
Tokibana Baw ), katibu mkuu wa shirikisho la Kiafrika la michezo huo ( Sahir Edo
) , na mhandisi ( Sharif Alerian ) katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki, pamoja na
mwenyekiti na wanachama wa baraza la uongozi wa shirikisho la Kimisri Ia mpira
wa vinyoya.
Michuano ya kibara imeshuhudia
kushiriki kwa nchi 14 nazo ni : Misri, Algeria, Morocco, Tunisia, Afrika
Kusini, Nigeria, Morishios, Sierra Leone, Zambia, Zimbabwe, Jamhuri ya
demokrasia ya Kongo, Cameron, Uganda na Botswana.
Comments