Waziri wa Michezo na raisi wa Al-Ahly waweka jiwe la msingi la Tawi la Kairo mpya
- 2020-02-17 11:39:21
Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, Mahmoud El-Khatib, Raisi wa baraza la wakurugenzi wa klabu ya Al-Ahly na Meja
Jenerali Ihab Al-Far, Mwenyekiti wa mamlaka ya uhandisi wa vikosi vya kijeshi,
Jumapili hii waliweka jiwe la msingi la tawi la Al-Ahly huko Kairo
mpya , kwa mahudhurio ya Al-Amri
Farouk, naibu mwenyekiti wa klabu ya Al-Ahly, Khaled Al-Dirandali, mweka
hazina, na wanachama wa klabu ya Al-Ahly.
Waziri wa Vijana na Michezo alielezea furaha yake kwa kuweka
jiwe la msingi la tawi jipya kwa Klabu ya Karne, akiashiria kuwa tawi jipya ni
ongezeko la nguvu katika vituo vya michezo vya Misri na bila shaka litachangia
kuandaa vizazi vya mabingwa wa michezo wanaoruka bendera ya Misri katika vikao
vya michezo mbali mbali.
Kwa upande wake, Mahmoud Al-Khatib alisisitiza furaha yake
kwa mahudhurio ya Waziri wa Vijana na
Michezo ili kuweka jiwe la msingi la
tawi jipya la klabu ya Al-Ahly , akisisitiza kwamba Waziri wa Vijana na Michezo
kila wakati ni msaidizi wa vifaa vipya vya michezo.
Al-Khatib ameongeza kuwa tawi jipya litakuwa ongezeko la
nguvu kwa Klabu ya Al-Ahly na wanachama wake katika kuhifadhi misingi, kanuni
na maadili.
Tawi la Al-Ahly huko
Kairo mpya ndilo tawi la nne la klabu baada ya tawi la Al-Jazeera, tawi
la Nasr City, na tawi la Sheikh Zayed .. Klabu ya Al-Ahly ilibuni tawi la klabu
katika mkutano wa tano na mpango wa jumla kulingana na miundo bora ya uhandisi
yanayokima mahitaji yote ya huduma za wanachama
na utekelezaji wa tawi unamalizika mnamo mwaka mmoja .
Sehemu ya ujumla kwa tawi la Al-Ahly huko Kairo mpya ni
ekari 50 na inajumuisha viwanja vikubwa viwili vya mpira wa miguu, viwanja 4
vya kikhomasia , viwanja 4 vya mpira wa mikono, viwanja 4 vya mpira wa wavu,
viwanja 4 vya mpira wa kikapu, viwanja 6
vya Tenisi na mkusanyiko wa mabwawa ya kuogelea yanayokusanya bwawa la
kuogolea la kiolimpiki, bafuni ya kupiga mbizi, ukumbi funiko, pamoja na jengo
la Boga, mabustani kwa wanachama, na eneo la michezo ya watoto.
Comments