Kuandaa kwa michuano ya kombe la mataifa ya
kiafrika..
"Urithi wa kienyeji wa kiafrika " umo juu
ya kuta za uwanja wa Aleksandaria.
Kwa vichoro vinavyoelezea urithi wa kienyeji wa
kiafrika, uwanja wa Aleksandaria ulianza kupamba kuta zake za nje ili
kuzikaribisha timu zinazoshirikiana katika michuano ya kombe la mataifa ya
kiafrika ya 32 ambao inakaribishwa hapa nchini Misri na itaanza kwa tarehe ya
21 Juni ujao. Na bwana Sherif
Saad"Mkurugenzi wa uwanja wa Aleksandaria "alisema kwamba vichoro
vinavyochorwa kwenye kuta za uwanja vinaelezea urithi wa kienyeji kwa nchi za
kiafrika, miongoni mwake kuna kichoro cha msichana mwafrika, na kingine
kinaelezea shughuli maarufu barani, na "Saad" mnamo kauli mahsusi kwa
Jarida la (ElAhram) aliongeza kwamba kampuni inayofanya shughuli za
maendeleo na mapambo ilipendelea kupamba
ukuta wa nje wa uwanja kwa( Grafiti), na kuchagua urithi wa kienyeji wa
kiafrika ili uwe kielezo bora zaidi kwa michuano, na bwana "Saad"
alieleza kwamba idara ya uwanja ndiyo iliyoamua wazo la vichoro vinavyochorwa,
na kwa kujibu juu ya malalamiko yaliyotolewa kwa vichoro bwana "Saad"
alisisitiza kwamba shughuli bado zinafanyika hadi sasa na inayoamuliwa ni
kumalizika kwa mwisho wa mwezi huu wa Mei, akithibitisha kwamba shughuli
hufanyikwa kwa juu na chini ili mkoa wa Aleksandaria uwe katika umbo lake la uzuri
mnamo michuano.
Comments