Misri inachukua nafasi ya kwanza kwa michuano ya Afrika ya mpira wa vinyoya kwa watu wazima
- 2020-02-18 12:18:49
Timu ya kitaifa ya kwanza kwa mpira wa vinyoya imechukua nafasi ya kwanza kwa michuano ya Afrika ya mpira wa vinyoya kwa watu wazima, iliyofanyika kwenye sebule namba 2 katika uwanja wa kimataifa wa Kairo mnamo kipindi cha tarehe 10 hadi 16, mwezi huu wa Februari.
Mafarao wamepata
nafasi ya kwanza katika mpangilio wa jumla baada ya ushindi wao kwa medali 8 ambazo ni : medali 3 za kidhahabu na
medali 5 za shaba, huku timu ya kitaifa ya Morishios imechukua nafasi ya pili
baada ya kushinda kwa medali 6 ambazo ni : medali mbili za kidhahabu, medali
mbili za kifedha na medali mbili za shaba.
Timu ya kitaifa ya
Algeria imekuja katika nafasi ya tatu kwa ujumla wa medali 4 ambazo ni : medali
mbili za kidhahabu na medali mbili za kifedha, huku timu ya kitaifa ya Nigeria
imechukua nafasi ya nne kwa medali 6 ambazo ni : medali 3 za kifedha na medali
3 za shaba, lakini timu ya kitaifa ya Afrika Kusini imechukua nafasi ya tano
kwa medali 3 za shaba, na mwishoni timu ya kitaifa ya Cameron imepata nafsi ya
sita kwa medali moja ya shaba.
Michuano ya bara
imeshuhudia kushiriki kwa nchi 14 nazo ni : Misri, Algeria, Morocco, Tunisia,
Afrika Kusini, Nigeria, Morishios, Sierra Leone, Zambia, Zimbabwe, Jamhuri ya
Congo ya kidemokrasia, Cameron, Uganda na Betswana.
Comments