Kabla ya safari yao kuelekea Morocco ... Waziri wa vijana na michezo anakutana na ujumbe wa Kimisri unaoshiriki katika michuano ya Afrika ya Taikondo

 Jumatano, Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo amekutana na ujumbe wa Kimisri unaoshiriki katika michuano ya Afrika ya Taikondo inayokaribishwa na Morocvo mnamo kipindi cha tarehe 21 hadi 24, mwezi huu wa Februari, na itakayofikisha  michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020, hii kwa mahudhurio ya Amr Selim  mwenyekiti wa shirikisho la Taikondo la Kimisri, na Mexico Oscar Salazar  mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya kitaifa, pia Hany Ali  mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya kitaifa ya Paralympic.


Wakati wa mkutano, Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo amesisitiza kuwa wizara ya vijana na michezo haijazuia juhudi zozote za kutoa misaada ya kila aina kwa wachezaji wote wa timu ya kitaifa ya Kimisri katika michezo yote ya riadha ya kibinafsi na ya pamoja kwa ajili ya kufikia majukwaa ya kutawaza kwenye viwango vyote vya bara, kimataifa na kidunia pamoja na kuinua bendera ya Kimisri juu yake.


Waziri wa vijana na michezo ametaka wachezaji wote kutia juhudi kubwa zaidi wakati wa mechi za michuano ili kuhakikisha ushindi na kufikia michezo ya Olimpiki.


Kwa upande wake, Amr Selim  mwenyekiti wa shirikisho la Taikondo la Kimisri akitoa shukrani kwa Waziri wa vijana na michezo juu ya misaada na uungaji mkono kwa shirikisho la Takondo la Kimisri.


Mwishoni mwa mkutano, Waziri wa vijana na michezo ameelezea matakwa yake ya mafanikio kwa wachezaji wote na wanachama wote wa ujumbe wa Kimisri.


Timu yetu ya kitaifa kwa Taikondo inawakilishwa na : Hedaia Malak, Seif Issa, Abdalrahman Wael na Nour Hussen.

Timu ya kitaifa ya Misri ya Paralympic inawakilishwa na : Mohamed Alzayat, Ahmed Albouhy, Amal Khalaf na Salma Ali.


Msaidizi wa waziri  Mohamed Alkordy na Naibu waziri Abd Alawal Mohamed wamehudhuria mkutano huo.

Comments