Chuo kikuu cha Helwan kinaainisha dhamini 40 za kimasomo kwa wanafunzi barani Afrika, Mashariki na Kusini mwa Asia na Amerika ya Kaskazini
- 2020-02-24 13:00:14
Chuo kikuu cha Helwan kimeainisha masomo ya kila mwaka kwa wanafunzi, ambapo Baraza la Chuo Kikuu lilikubali kuainisha dhamini 40 za kimasomo katika taaluma mbalimbali kwa ngazi za shahada ya kwanza na masomo ya juu kwa mwaka 2020/2021, na katika shime ya chuo kikuu cha Helwan kinachoongozwa na Dokta Majed Najm, Rais wa Chuo Kikuu na uongozi wa Dokta Mona Fouad Attia, Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu kwa Mafunzo ya juu na utafiti kwa kupatikana upeo mpya wa ushirikiano na nchi za Kiafrika, Mashariki na Kusini mwa nchi za Asia, na nchi za Amerika ya Kaskazini, kuunga mkono ushirikiano na urafiki, na kuimarisha mahusiano wa kihistoria.
Dokta Majed Najm, Rais wa Chuo Kikuu hicho, alielezea kuwa
misaada hii inakusudia kupatikana nafasi
mpya za kisayansi na nchi tofauti kwa madhumuni ya kufanikisha maendeleo ya
kisayansi na kiteknolojia kwa kuzingatia taaluma za kipekee zinazokuwepo
pale Chuo Kikuu cha Helwan na mipango
iliyotofautisha inayokidhi mahitaji ya soko la ajira la kikanda na kimataifa na
kusisitiza jukumu la kitamaduni na kitaalam la Misri na msaada wa njia za
ushirikiano wa kisayansi pamoja na nchi
tofauti.
Kwa upande wake, Dokta Mona Fouad Attia, Makamu wa Rais wa
Masomo ya juu na Masuala ya Utafiti alionyesha kuwa idadi ya dhamini
zinazotolewa kwa chuo kikuu itaongezeka kila mwaka katika nyanja mbalimbali na
katika fani zote, ambapo chuo kikuu
kinawakaribisha wanafunzi wa nje na kuwapa msaada wote, akibainisha kuwa Kituo
cha Masomo na Ushirikiano wa utafiti wa Afrika kimejitolea kwa mwaka wa kwanza
Udhamini wa Uzamili wa kusoma usimamizi
wa maeneo ya kiutalii kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya utalii kwa ngazi ya kienyeji na kikanda barani.
Kwa upande mwengine, Sekta ya Mafunzo na Utafiti ya Uzamili
katika Chuo Kikuu cha Helwan chini ya
uongozi wa Dokta Majed Negm, Rais wa Chuo Kikuu na Dokta Mona Fouad Attia,
Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Uzamili na Utafiti ilipanga semina
juu ya maendeleo ya majarida ya kisayansi katika vyuo vikuu vya kimisri, na hiyo ni wakati wa shime ya Chuo Kikuu cha Helwan katika utafiti wa
kisayansi na uchapishaji wa kimataifa kwa lengo la kukiweka chuo kikuu cha
Helwan katika safu ya uainishaji wa kimataifa kwa vyuo vikuu vya ulimwengu.
Comments