Shirikisho la kiafrika la Taikondo linaandaa michuano ya Kombe la Rais huko Aswan Desemba ijayo

 Meja Jenerali Ahmed El-Fouly, Rais wa Shirikisho la Afrika la Taikondo na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Dunia, walitangaza kwamba mji mmisri wa Aswan utaikaribisha  michuano ya Kombe la G2 la Rais Desemba ijayo, baada ya Côte d'Ivoire iliomba msamaha kwa kukaribisha michuano .

 El-Fouly alisema kuwa Rais wa Shirikisho la kimataifa la Taikondo Dokta Chung Wan Shu, alikuwa ameichagua Misri ili kukaribisha mashindano hayo, kwa sababu ya imani yake katika Shirikisho la kiafrika kwa mchezo huo, litakaloandaa mashindano hayo nchini Misri.

El-Fouly ameongeza kuwa  michuano ya Kombe la Rais inachukuliwa kuwa moja ya mashindano ya kimataifa yenye nguvu na inategemewa kwamba idadi kubwa ya nchi tofauti zitashiriki,  inayochangia kufufua upya utalii wa kimichezo na inaambatana na mwelekeo wa nchi ya kimisri inayoongozwa na Rais Abd El  Fatah El-Sisi, na Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo katika kuunga mkono hafla  kubwa za michezo baada ya kugeuza  Misri na iwe kama mwelekeo kwa kupokea matukio ya bara na kimataifa.

El-Fouly alimaliza matamshi yake, akiwataka viongozi wanaohusika na Wizara ya Vijana na Michezo kutoa msaada wa kutosha katika kuandaa michuano ya dunia inayofaa kwa jina la Misri .

Comments