Hedaia Malak mchezaji wa Taikondo anafikia olimpiki ya Tokyo

 Hedaia Malak mchezaji wa timu ya kitaifa ya Taikondo alifikia duru ya michezo ya olimpiki ya Tokyo baada ya kushinda kwake katika  mechi ya nusu fainali kwa mchezaji wa kenya Alosh Everlin kwa  30-4 wakati wa fainali ya kiafrika kwa Taikondo inayofikisha olimpiki na inayofanyika hivi sasa katika mji wa Rebat wa Morocco

 

Na baada ya kushinda kwake katika mechi ya nusu fainali , Hedaia alihakikisha kadi ya olimpiki ambapo wachezaji wawili wa kwanza wa kila uzani wanafikia duru ya michezo ya olimpiki

 

Na Misri  inacheza mashindano kwa wachezaji wanne (wanawake wawili na wanaume wawili) na wachezaji wanaume ni Abdelrahman Wael katika mashindano ya uzani wa  kg -68 na Seif Eissa katika mashindano ya uzani wa kg -80 na wachezaji wanawake ni Nour Hussien katika mashindano ya uzani wa kg -49 na Hedaia Malak katika mashindano ya uzani wa kg -67

 

Timu ya kitaifa ya Misri  inaongozwa na kocha wa kiufundi wa Mexico oskar salazar na makocha wawili  Osama Elsayed na Mohammed Magdy

Comments