Waziri wa Michezo anasaini itifaki ya ushirikiano pamoja na Maktaba ya Alskandaria kwa kuwafundisha na kuwawezesha vijana
- 2020-02-27 11:24:08
Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, amekutana na kikundi cha vijana wa vyuo vikuu vya kimisri, kwa mahudhurio ya Dokta Mustafa El-Feki, Mkurugenzi wa Maktaba ya Aleskandaria, na hiyo kwa ajili ya kusikiliza maoni na mapendekezo ya vijana katika hatua ya kisasa, ambapo mkutano huo unahudhuriwa na vyama vya wanafunzi katika vyuo vikuu vya kimisri na taasisi za juu, na Jumuiya ya Wanafunzi waafrika chini ya kauli mbiu ya "nguvu za vijana kwa siku zijazo."
Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza umuhimu wa kusikiliza kabisa maoni na mawazo ya vijana na msaada wao kwani wanawakilisha sehemu kubwa zaidi ya jamii ya kimisri, na nchi imekuwa ikitegemea sana maoni na mapendekezo yao katika kuendeleza nchi kwa kufaidika na maoni yao na kutekeleza mazuri na yanayofaa maishani.
Pia Sobhy alisaini itifaki ya ushirikiano kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Maktaba ya Alskandaria kwa ajili ya kuwafundisha na kuwawezesha vijana na kufanya kazi ili kuinua uwezo wao katika nyanja zote ambapo itifaki inatoka kwa kuzingatia jukumu la Wizara ya Vijana na Michezo na hamu yake ya mara kwa mara ya kushirikiana na taasisi tofauti zinazowasaidia vijana, na kuwapa njia nyingi za mafunzo na uwezeshaji. Kwa maisha bora ya baadaye.
Pia Dokta Ashraf Sobhy alionyesha kuwa Wizara ya Vijana na Michezo ndio mamlaka inayohusika na kuboresha maisha ya vijana wamisri kwa kuchukua mipango ya vijana na michezo iliyofanikiwa, na kufanya kazi ya kuzitokwa ili kuteklezwa pamoja na kupanua ushirikiano wa jamii na taasisi za kazi za umma, kwa kuzingatia msaada unaoendelea kutoka kwa Rais Abd El-Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.
Inapasa kuzingatia kwamba vifungu vya itifaki hiyo ni pamoja na mafunzo na uwezeshaji wa vijana, pamoja na kuteua Makada wachanga kushiriki na mafunzo ya vitendo, na kuweka mipango ya pamoja kati ya Wizara na maktaba, programu husika katika kuongeza ufanisi wa vijana, na pia kutoa fursa ya kufanya maonyesho ya bidhaa za urithi na vijana kupitia klabu za wasichana katika vituo vya vijana.
Semina hiyo ilihudhuriwa na Profesa Nagwa Salah, Naibu wa Wizara , Mkuu wa Idara kuu kwa Programu za Utamaduni na Hiari, Dokta Safaa Al-Sharif, Naibu wa Wizara , Mkurugenzi wa Kurugenzi la Vijana na Michezo huko Aleskandria, Bibi Manal Ismail, Mkurugenzi Mkuu wa Mahusiano ya Umma na vyombo vya Habari katika Kurugenzi la Vijana na Michezo huko Aleskandria, na Idadi ya wajumbe wa bodi ya idara ya maktaba ya Aleksandria.
Comments