Patrice lumumba Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, na yeye ni
miongoni mwa wale ambao walioacha athari kubwa katika historia ya sasa ya
Afrika, kwani yeye alijitolea maisha yake katika mapambano ya kuwakomboa watu
wa Kongo katika harakati za kugombea uhuru kutoka utawala wa kikoloni pamoja na juhudi zake
zilizofanyika katika kuanzisha wazo la Umoja wa Mataifa ya Kiafrika na kwa
mantika hii alishiriki katika mkutano wa
Umoja wa Mataifa ya Kiafrika uliofanyika mjini Accra nchini Ghana mwaka 1958 na
alikutana na hayati Kwame Nkrumah.
Na inaelezwa kwamba mkutano huo ulizungumzia kwa kina wazo
la Umoja wa Kiafrika katika ufahamu wa
Kikongo na uhusiano wake mzuri na viongozi wengine wa kiafrika kama vile Jamal
Abdul-Nasir, Ahmad Siku Toure na Kwame Nkrumah. Na mapambano ya Lumumba katika
harakati za kugombea uhuru kwa Kongo
toka kwa utawala wa kikoloni unaandikwa
kwa maji ya dhahabu katika kurasa za historia ya sasa ya Afrika na pia uvutiaji
wake ulienea katika nchi yake na nchi za nje na kuenea bara zima la Afrika.
Lakini kwa sababu ya uwepo wake katika maeneo yote ya mapambano yenye lengo
la uhuru wa nchi yake ulimfanya
kukamatwa mara kwa mara na kuwekwa gerezani.
Na kanuni ambazo zilipambanua mapambano yake katika
kufanikisha uhuru zilikuwa na sifa ya amani, zisizo na vurugu zenye ujasiri na
nguvu ili kufanikisha haki ya kijamii na alikataa uwepo wa ukuloni na uporaji
wa mali za nchi za Kiafrika na aliashiria kwamba “vita ambavyo tunavipata
kutoka tawala za kikoloni chini visingizio dhaifu na kwa madai ya kupiga
vita ukomunisti vinaficha makusudio ya
kweli yasiyotangazwa kwani tawala hizo za kikoloni hazina huruma ila kwa
wafuasi wao kutoka viongozi wa kiafrika ambao wamewasaliti watu wao. Na
hawaleti kwa nchi zetu za Afrika ila uporaji wa mali zetu kwa kula njama na
viongozi hao mafisadi”.
Na Patric Lumumba
aliuliwa kwa amri ya Wakoloni tarehe 17 Januari mwaka 1971 akiwa na umri
wa miaka 53, lakini amebaki kuwa ni kiongozi imara katika historia ya sasa ya Afrika kwa
kutambua mapambano yake na misimamo yake ya heshima.
Comments