Enye ndugu, wana wa
Afrika mpendwa ndani ya bara letu mama na katika pembe zote za ardhi.
Kila mwaka na
nyinyi mpo salama na wenye kheri kwa mnasaba wa siku ya Afrika.
Nawazungumzeni leo ili kuwapongeza kqa mnasaba
wa siku ya Afrika.... Kumbukumbu ile ya kihistoria iliyoshuhudia uanzishi wa
shirikisho la umoja wa kiafrika, pia iliyounda zama mpya kwa shughuli za
ushikamano wa kiafrika na kuimarisha shughuli ya pamoja kati ya nchi za bara
letu pendwa.
Basi kwamba
tangu miaka 56 katika siku hii hii, baba
waanzishi wa shirikisho la Umoja wa kiafrika waliweka mizizi ya umoja na
ushirikiano wa kiafrika, pia waliweka mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi na
ukamilifu wa kibara, na waliunda njia sahihi za kulipitisha bara la Afrika
kuelekea utulivu, maendeleo, na ustawi.
Nasi leo
tunapata tija za juhudi za baba waanzishi wa shirikisho la umoja wa kiafrika,
na kuunda vijana waafrika kwa utaratibu na uendelevu mnamo miongo iliyopita,
basi bara letu pendwa linaelekea kwa utulivu kwa kuhakikisha maendeleo endelevu
kupitia kutekleza mpango wake mwenye matarajio maalumu unaowakilishwa katika
Ajenda ya 2063,na siku kwa siku shughuli za juhudi zetu za pamoja zinaongeza
kusuluhisha mizozo na matatizo yaliyokabili bara kwa miongo kadhaa na yalizuia
kuhakikisha ndoto za wananchi wake.
Na ili
kuhakikisha malengo yetu ya pamoja.... Lazima kupata faida toka uwezo wa sekta
binafsi, pamoja na juhudi za serikali za kiafrika, na hayo yote yakisisimua
vijana waafrika kwa kujenga miradi mikubwa zaidi kwa bara ili kuboresha mfumo
wa miundombinu ya kiafrika, linalochangia kukamilisha shughuli za uchangamano
wa kikanda, ukamilifu wa kiuchumi, na kuunganisha masoko ya kiafrika, na pia
linasaidia kutekleza mkataba wa biashara huru ya kibara ambao sote pamoja
tunajiandaa kuutekleza mnamo kilele chetu cha mara kitakachoundwa mnamo mwezi
wa Julai ujao kwenye Jamhuri ndugu ya Naiger.
Na kwa
kusawazisha pamoja na juhudi maendeleo haya..
Tunapaswa kuhangaika kuboresha Rasilimali zetu za binadamu, kuwawezesha
vijana wa bara kwa kuendelea na maendeleo ya zama na kuwaelimisha majukumu yao
ya kuiongoza mustakbali ya bara la Afrika... Pamoja na kuendelea kuimarisha
mchango wa mwanamke mwafrika kama chombo
muhimu kwa jamii zake na nguzo kwa mageuzi yake ya kiuchumi na utulivu wake,
pamoja na kuunganisha mielekeo ya
kiutamaduni na kiustarabu kati ya nchi zetu, kuuthibitisha utambulisho wetu wa
kiafrika na kuongeza misingi ya ushikamano wa kiafrika.
Ndugu zangu,
hatuna budi ila kutia juhudi na kuhifadhi Umoja wetu ili kuhakikisha ndoto ya
baba waanzishi, na matarajio ya wananchi wa bara adhimu la Afrika kwa
kupatikana bara lenye utulivu, lenye ustawi, na linadhamini maisha ya ukarimu
kwa wana wake wote, na kutia mwanga wa ustarabu, ufahamu wa usamehe, na upendo
kwa ulimwengu wote.
Na bara letu
lina mahusiano mengi ya kushirikiana pamoja na washiriki wote wa mataifa,
kutoka serikali, taasisi za kitaifa, kampuni za sekta binafsi, na mashirikisho
ya kifedha ya kimataifa kwa kujenga Afrika linalotarajiwa.. Na hayo yote ni
kupitia ushirikiano na shughuli za kimaendeleo zinazodhamini kuhakikisha
maslaha kwa pande zote kwa uadilifu, pia kuchangia kuimarisha utulivu, ustawi
wa ulimwengu wetu, na kuzidisha majaribio ya binadamu.
Na
mwishoni.... Kila mwaka na Afrika ni
lenye ushikamano mkubwa zaidi, ushirikiano wa kina na lenye ukamilifu
kamili..... Kila mwaka na nchi za Afrika
kwa pambe zake zote zipo ndani ya unganisho, ustawi, na utulivu.
Asanteni sana.
Salamu ,
rehema, na baraka za Mwenyezi Mungu juu yenu. ( Alsalam Alykum Warahmat Allah
Wabarakatu).
Comments