Itifaki ya ushirikiano kati ya shirikisho la kimisri na la ulimwengu kwa Elkhomasi ya kisasa kwa ajili ya kuyapokea Mashindano ya Ulimwengu ya Vijana ya mwaka 2021

Mkurugenzi wa Shirikisho la Kimisri la Elkhomasi ya kisasa Sherief Al-Aryaan, mkurugenzi wa tasisi ya kiarabu kwa sayansi na teknolojia na usafiri wa baharini Esmail Abd-Alghafour na mkurugeni wa Shirikisho la Kimataifa la Elkhomasi ya kisasa Klaus Schurman, wametilia saini ya itifaki ya ushirikiano ili kuyakaribisha mashindano ya ulimwengu ya vijana ya mwaka 2021 na hivyo kwenye  uwanja wa taasisi ya mjini Aleskandaria.

Al-Aryaan ameeleza furaha yake kwa kutilia saini itifaki hiyo, inayozingatia imani ya shirikisho la ulimwengu katika uwezo wa  Misri kwa udhibiti.  Na akielekea shukuru yake kwa Dokta Esmail Abd-Alghafour kwa msaada wake kwa mchezo wa Elkhomasi ya kisasa na kuyakaribisha  mashindano muhimu ya Shirikisho la Kimataifa.

Kwa upande wake, Klaus Schurman,  Mkurugenzi wa shirikisho la Kimataifa, aliashiria kwa nafasi ya kipekee ya Misri katika mchezo wa Elkhomasi ya kisasa kupitia wachezaji, uwezo wa udhibiti na ujuzi bora zaidi, ambayo imefanya Misri kituo cha kimsingi katika kuandaa mfululizo wa Kombe la Ulimwengu. akitarajia uandaaji mzuri sana kwa Kombe la Ulimwengu kwa Vijana kwa mwaka 2021.

Na pia Esmail Abd-Alghafour, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kirabu, akasisitizia kutoa misaada yote ili mashindano hayo yaonekane kwa njia inayofaa jina la kimichezo la Misri. Na akizingatia juu ya umuhimu wa uungaji mkono kwa mashindano yaliyofanyika nchini Misri.

Comments