Waziri wa michezo akijadiliana , Hassan Mostfa na kamati iandaayo maelezo ya kutangaza michuano ya dunia kwa mpira wa mikono
- 2020-03-04 17:55:24
Dokta Ashraf Sobhy waziri wa vijana na michezo alifanya mkutano mkubwa pamoja na Dokta Hassan Mostfa mkuu wa shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono na wanachama wa kamati iandaayo michuano ya kombe la dunia kwa mpira wa mikono 2021 , wakilishi wa runinga ya kimisri na kampuni ya presintation ili kujadili idhaa ya runinga na haki zake kwa michuano ya kombe la dunia kwa mpira wa mikono 2021 , na wanachama kutoka kampuni ya Logarder yenye haki ya kuitangaza michuano .
Mkutano ulijadili mazungumzo juu ya haki za kutangaza na gharama maalum za kupata Misri haki za kutangazia kwenye runinga ya kitaifa na ya
Sputniki kwa mechi za michuano .
Sobhy alitia tamaa juu ya hatua zinazofanywa kwa ajili ya kujiandaa ili kukaribisha michuano ya kombe la dunia kwa mpira wa mikono akielezea kwamba wizara ya vijana na michezo inafanya daima mapatano kati ya pande zote zinazohusika kwa ajili ya kufanya michuano inayofaa kwa jina la Misri na ulimwenguni .
Vilevile, alitoa shukrani zake kwa Dokta Hassan Mustafa mkuu wa shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono juu ya kufanya mkutano wa baraza la usimamizi wa shirikiano la kimataifa nchini Misri kwa mara ya kwanza utakaofanywa mnamo siku chache zijazo .
Akiongeza kuwa kukaribisha Misri kwa michuano ya kombe la dunia kwa mpira wa mikono ni tukio muhimu na ya kipekee kabisa kuliko michuano mengine hasa toleo hili linazingatia kuwa la kwanza katika kombe la dunia linalojumuisha timu 32 ambapo Dokta Hassan Mostfa mkuu wa shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono alitoa shukrani juu ya kupokea mkutano ,akisifu mapatano ya kudumu kati ya wizara ya vijana na michezo na mashirikiano ya Kimisri na kimataifa kwa mpira wa mikono kwa ajili ya kufanya michuano ya kombe la dunia la mpira wa mkono kwa ufanisi .
Na kwa upande wake , " Naala Farouk " mkuu wa sekta ya televesheni ya kimisri alifafanua kuwa Runinga ya kimisri inakaraibia kupatikanisha magari manne ili kutangaza kwa mbinu wa 4k, vilevile ,Inayopangwa kufanya mazoezi mara kwa mara kwenye viwanja vinavyochezwa michuano ndani yake pia ameahidi kuwezesha huduma bora zenye mbinu za juu kwa ajili ya kuonesha kufuatilia bora kwa michuano kwa hadhira za Kimisri na kimataifa .
Mkutano ulihudhuriwa na Nahla farouk mkuu wa sekta ya runinga ya Kimisri , mhandisi Hisham Nasr mkuu wa shirikianzo la Kimisri kwa mpira wa mikono , mhandisi Hussian Labib mkuu wa michuano ya kombe la dunia kwa mpira wa mikono 2021 , drokta Ahmed Elshekh mkuu wa usimamizi mkuu kwa mambo ya ofisi wa waziri wa vijana na michezo , Bwana Zaky Abd Elhamed Naibu wa mkuu wa baraza la usimamizi wa kampuni ya prisention , Bwana Kamal Elden Mahmoud mkuu wa usimamizi mkuu wa Bajeti ya kabati ya fedha kwa wizara ya fedha na Mshauri Mouhmed Deiab mshauri wa sheria kwa wizara ya vijana na michezo .
Comments