Waziri wa michezo analipongeza baraza la Shirikisho la Tenisi ya mezani kwa kufikisha Misri kwa michezo ya Olimpiki mjini Tokyo
- 2020-03-04 18:05:45
Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo amelipongeza baraza la shirikisho la Kimisri kwa Tenisi ya mezani chini ya uongozi wa Moataz Ashour juu ya kufikisha Misri kuelekea michezo ya Olimpiki kwa alama kamili.
Sobhy amesifu utendaji wa kiufundi wa kipekee ambao wachezaji wameufanyika kutoka watu wawili ambao ni : Omar Asar na Dina Moshref katika kuhakikisha nafasi ya kwanza ya fainali za Kiafrika zinazofanyika nchini Tunisia na zitakazofikisha Tokyo 2020 baada ya ushindi juu ya Djibouti 4/0, kisha Tunisia 4/0, kisha Nigeria 4/0.
Sobhy ameelezea furaha yake kwa ufikiaji wa kipekee kwa timu ya Tenisi ya mezani ya kimisri, akisisitiza kuendelea kwa uungaji mkono kwa wachezaji, akiashiria matarajio yake makubwa kwa kuhakikisha mafanikio makubwa kwa riadha ya Kimisri katika michezo ya Olimpiki ya Tokyo pamoja na kuandika historia ya michezo kwa mabingwa wa Misri wa michezo katika michezo mbalimbali.
Imetajwa kuwa Misri ilikuwa imefikia katika mashindano ya timu na ya kibinafsi wakati wa kikao cha michezo ya Kiafrika huko Morocco, timu ya Kimisri itashiriki kwa wachezaji 6 ambao ni : Omar Asar, Ahmed Saleh, Khaled Asar, Dina Moshref, Yossra Helmy na Farah Abd Alaziz. Chini ya uongozi wa wafanyikazi ya kiufundi kwa timu ya kitaifa : kocha Maged Ashour mkurugenzi wa kiufundi kwa wanaume na kocha Ashraf Helmy mkurugenzi wa kiufundi kwa wanawake.
Comments