Waziri wa Vijana na Michezo akihudhuria mkutano wa ufunguzi wa Mkutano wa Kiarabu kwa Michezo na Sheria
- 2020-03-04 18:14:34
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo jumanne alishuhudia ufunguzi wa Mkutano wa Kiarabu wa Michezo na Sheria, chini ya anwani ya "Kusimamia utatuzi wa mizozo ya michezo kati ya mahakama na usuluhishi", ulioandaliwa kwa Kamati ya Olimpiki ya kimisri kwa kushirikiana na Shirikisho la Kiarabu la Maendeleo ya mkusanyiko wa Nchi za Kiarabu.
Mkutano huo, uliofanyika katika makao makuu ya Shirika la Maendeleo ya kitawala wa Kiarabu, ulihudhuriwa na Dokta Hassan Mostafa Rais wa shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono na mwanachama wa ofisi ya kiutendaji kwa kamati ya kimataifa ya olimpiki na Mhandisi Hisham Hatb rais wa kamati ya olimpiki ya kimisri , Dokta Nasser Elhatlan Elkahtanh mkurugenzi mkuu wa shirika la maendeleo la kiutawala wa nchi za kiarabu idadi ya wataalamu wa Michezo ya Misri , wakuu wa mashirika ya michezo, wakuu wa klabu, na wataalam wa kisheria kutoka Misri, na kikundi cha watu wa Kiarabu na wakilishi kutoka Saudi Arabia, Emirates, Morocco, Algeria, Palestina, Yemen, Libya, Bahrain na Iraq.
Mkutano huo ulijadili pointi kadhaa zinazohusiana na usuluhishi na uhusiano wake na michezo, mikataba na uwekezaji wa michezo, kujadili uzoefu wa Misri katika usuluhishi wa michezo na kusoma jinsi ya kuunda shirika la Waarabu kwa usuluhishi wa michezo.
Mkutano huo ulifunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Kiarabu la Maendeleo ya kiutawala, ambapo alisisitiza kwamba kuanzishwa kwa mkutano huo ni jambo muhimu katika michezo ya Kiarabu, inayohitaji kufafanua umuhimu wa sheria za michezo, akisema kwamba shughuli za mkutano huo zinashuhudia mjadala na ufafanuzi wa mambo mengi muhimu kuwa na mchezo uliopangwa na wenye mafanikio, akitoa shukrani na uthamini Kwa mratibu wa kisayansi wa mkutano huo, Mshauri Ayman Abd El Rahman,naibu wa Rais wa Mamlaka ya Masuala ya Nchi na Mshauri wa Sheria kwa Kamati ya Olimpiki ya kimisri.
Katika hotuba yake, Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kwamba usuluhishi wa kimichezo ni moja ya misingi muhimu ya mafanikio, hasa kuwa inaweka muundo na mipaka ya ushindani halali ndani ya uwanja wa michezo, akionyesha kuwa majadiliano na maendeleo ya sheria na usuluhishi wa kimichezo huongeza nafasi za ushindani waaminifu na kuchangia kwa kiasi kikubwa kufanikiwa.
Waziri wa Vijana na Michezo aliwashukuru washiriki wote katika mkutano huo kwa ajili ya kujadili jukumu la usuluhishi wa kimichezo katika kusuluhisha mizozo ya michezo, akisisitiza kwamba serikali ya kimisri iliyowakilishwa katika Wizara ya Vijana na Michezo inaunga mkono sheria ya michezo na umuhimu wa kuwepo kwake.
Wakati ambapo Mhandisi Hisham Hatab alisema: "Mchezo wa kimisri unashuhudia kiwango kikubwa juu ya kiwango kiutawala , riadha na kisheria kwa kuzingatia ushirikiano kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Kamati ya Olimpiki ya kimisri na juhudi za Dokta Hassan Mustafa, Rais wa Shirikisho kwa Mpira wa mikono la Kimataifa." Akiongeza kuwa leo tunasimama mbele ya hatua muhimu katika historia ya michezo. Ni majadiliano juu ya umuhimu wa sheria za michezo na jukumu ambalo sheria imechangia katika kuanzisha utulivu na maendeleo ya michezo ya Misri, ikizingatiwa kwamba mkutano huu ni hatua ya kufafanua uzoefu wa Misri na mawasiliano ya Waarabu kwa siku zijazo bora kwa sheria za michezo.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikono alifafanua kuwa wazo la mkutano huo ni muhimu na kuelezea umuhimu na jukumu la sheria ya michezo na falsafa ya usuluhishi wa michezo na kwamba kanuni zinazosimamia michezo ni sehemu muhimu ya michezo na njia hii inaambatana na kanuni za michezo za kimataifa na michezo ina jukumu kubwa katika maisha ya mataifa na baada ya michezo kugeuka kuwa bidhaa Uwekezaji mkubwa ambao unapaswa kuendana na kanuni na sheria za michezo zinazoongoza shughuli za michezo.
Dokta Hassan Mustafa alisisitiza juu ya umuhimu wa kuwepo kwa vituo vya usuluhishi, ambavyo vitasimamia uhusiano kati ya watu na mashirika ya michezo , akisema kwamba Mkataba wa Olimpiki ulizingatia vitu vinavyoelezea uhusiano huo kwa nia ya kuongeza jukumu la vyama vya umma, ukizingatia wakati huo huo kwamba sheria ilitolewa kwa masilahi ya jumla na haikujali watu Moja hasa, kama wengine wanavyorudia, ambayo iliipa makusanyiko ya jumla kuweka kanuni badala ya kuwa mikononi mwa mtu mmoja aliyeyadhibiti, wakati serikali kuhifadhiwa haki ya udhibiti wa kifedha.
Comments