Kwa maendeleo ya juhudi za Misri ya Kiafrika, Wizara ya Vijana na Michezo (Idara kuu kwa Bunge na elimu ya Kiraia na Ofisi ya Vijana wa Afrika) inayoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, kwa kushirikiana na Shirikisho la Vijana wa kiafrika, inatangaza kuzinduliwa kwa fomu kwa kushiriki katika kikundi cha pili cha Shule ya Kiafrika 2063, miongoni mwa Programu ya Uelewa wa Kiafrika katika toleo lake la sita, kinachotekelezwa mnamo Kipindi cha 25 hadi Aprili 5, 2020 huko Kairo.
Shule hiyo ndiyo ni nafasi ya mkutano wa viongozi wakuu wakiutendaji kwa sekta za nchi, sekta binafsi na Jamii ya kiraia katika muktadha wa kuandaa makada wa kiafrika kulingana na ilivyosisitizwa na Rais Abd El Fatah El-Sisi wakati wa Mkutano wa Vijana wa Ulimwengu na mkutano wa kilele cha Umoja wa Afrika mnamo Februari 2020.
Programu hiyo inalenga asilimia 50 ya Viongozi wa vijana waafrika wamisri kutoka kote nchini na asilimia 50 ya makada wa vijana waafrika wasio wamisri , kutoka wanafunzi, wanadiplomasia, na vijana wakimbizi. Hasa vijana wanaozungumza Kiarabu, pamoja na 5% kinachohusika kwa watu wenye uwezo maalum.
Programu hiyo inakusudia kuwaandaa viongozi vijana wenye imani kwa dhana ya umoja wa Kiafrika, kutambulisha Hati ya Vijana wa Kiafrika, kujihusisha vijana waafrika wasio wamisri katika jamii ya kimisri, kujihusisha wakimbizi kwa njia nzuri kupitia elimu inayoingiliana, kutambulisha na kuunganisha Maoni ya Misri 2030 ya kitaifa – na Ajenda 2063 barani - malengo ya maendeleo endelevu 2030 katika kiwango cha kimataifa na maendeleo ndani ya bara la Afrika, kuimarisha viunganishi vya kitamaduni, kijamii na kihistoria kupitia elimu miongoni mwa vijana wa nchi za Kiafrika, kuonyesha mchakato wa kufanya maamuzi katika Umoja wa Afrika, kuchora mkakati wazi wenye lengo la Kubadilisha taswira ya kidhahania ya bara la Afrika kwa wananchi wake , pamoja na kuarifu jukumu la taasisi na mashirika ya Kiafrika na kukuza ufahamu wa waafrika wenyewe katika hali ya kiutamaduni na kisanaa.
Kuhusu ushiriki na njia ya uwasilishaji, itakuwa kupitia kujaza fomu hii:
https://docs.google.com/…/1FAIpQLSf6GVe02uWEWtFtYg…/viewform
Comments