Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, alimpokea Dokta Anisa Hasouna, mwanachama wa Bunge , kwa ajili ya kujadili maelezo ya uzinduzi wa mpango wa "Moyo mwaminifu", unaojumuisha kuongeza uhamasishaji kutoka wanariadha, vijana kwa Taratibu za urekebeshaji wa moyo katika tukio la shida wa moyo na afya wakati wa hasa wakati wa mafunzo, shughuli na mashindano ya michezo.
Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kwamba mpango huo na shughuli zake zitazinduliwa wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Klabu ya "Alnady", inayopangwa kufanyika kesho, mjini 6 Oktoba na katika Kituo cha Vijana cha Gezira.
Waziri wa Vijana na Michezo aliashiria kuwa ramani ya muda na sehemu itatekelezwa ambapo itajumuisha vituo vyote vya vijana vilivyotawanyika katika vijiji vyote na miji ya mikoa ya Jamhuri kwa ajili ya kutekeleza mipango na vilabu vya michezo katika mikoa tofauti.
Kwa upande wake, Dokta Anisa Hasouna alieleza kuwa itifaki ya ushirikiano itakayofanyika wakati wa uzinduzi wa mpango huo itakuwa kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Hospitali bure ya Watu kwa magonjwa ya moyo kwa watoto, akiashiria kuwa Wizara ya Vijana na Michezo ina rasilimali za watu na mahali pia ambapo hueneza sana katika mikoa yote, inayoisaidia kueneza mpango huo itakayofaidi idadi kubwa ya vijana , hasa wanariadha wanaofanya michezo mara kwa mara, sawa na katika kiwango cha mazoezi au taaluma.
Comments