chini ya uangalifu wa Waziri mkuu , waziri wa vijana na michezo ashuhudia sherehe ya kumpongeza Hasan Mostafa mkuu wa shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono kwa ajili ya mwenendo wake na mafanikio yake
- 2020-03-09 11:48:04
Kwa niaba ya Dokta Mustafa Madbouly, Waziri Mkuu, Dokta
Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia
Sherehe ya kumheshimu Dokta Hassan Mustafa, Rais wa
Shirikisho la kimataifa kea Mpira wa
Mikono, lililofanyika chini ya matakwa
ya Waziri Mkuu na shirika la Kamati ya Olimpiki ya Misri na vyama vya michezo,
kwa mahudhurio ya Hisham Hatab, Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, Brigadier
Hazem Ibrahim, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Michezo ya Jeshi, Dokta Hayat Khattab,
mkuu wa Kamati ya Paralimpic ya Misri, Hisham Nasr, rais wa Shirikisho la kimisri kwa Mpira wa Mikono na kundi la
washiriki wa familia ya michezo ya kimisri.
Sherehe za kuheshimu ilikuwa pamoja na hotuba kadhaa, video
fupi juu ya mafanikio ya Dokta Hassan Mostafa, Rais wa Shirikisho la kimataifa
kwa Mpira wa Mikono,
Video kuhusu mafanikio ya uwekezaji wa michezo katika
michezo ya mtu mmoja, pamoja na kumheshimu Dokta Hassan Mostafa, Rais wa
Shirikisho la kimataifa kwa Mpira wa
Mikono aliyeheshemiwa kwa nishani tatu, ya kwanza ni nishani maalum, na nishani
imehifadhiwa kwenye Jumba la Olimpiki, na heshima ya tatu ni nishani ya urais
wenye heshima kwa Dokta Hassan Mostafa kwa Kamati ya Olimpiki ya Misri kwa
maisha yote .
Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, alisema:
Tunajivunia mtaalam wa michezo ya kimisri, Dokta Hassan Mostafa, ambaye ni
ishara kubwa kwa michezo ya Kimisri, na tunathamini uongozi wake kwa mchezo wa mpira wa mikono katika kiwango cha
kimataifa, na leo heshima yake ni hatua
thamini sana kwa mahudhurio ya
jamii ya michezo wakithamini mwenendo wa kutoa na mafanikio aliyoyahakikisha.
Katika hotuba yake, Dokta Hassan Mostafa aliwashukuru
washiriki wa familia ya michezo kwa heshima hii, akionyesha njia ya maisha yake
tangu alikuwa mchezaji, halafu kocha, halafu rais wa Shirikisho la kimisri kwa Mpira wa Mikono na kisha rais wa
Shirikisho la Kimataifa, na vizuizi alivyoyakabili kwenye maandamano hayo,
ambapo alivishinda kupitia utashi na uvumilivu.
Dokta Hassan Mostafa alimshukuru na kumthamini Dokta Ashraf
Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo kwa kukumbatia michezo ya Kimisri,
akiashiria ushirikiano wa kina kati ya
Wizara na Kamati ya Olimpiki ya Misri, ambayo inachangia maendeleo na mafanikio
ya michezo ya kimisri.
Kwa upande wake, Hisham Hatab, Rais wa Kamati ya Olimpiki ya
kimisri, alisema kwamba Dokta Hassan
Mostafa ni bingwa mzuri na ishara ya kweli ya kitaifa ambaye ana kiburi
kwa nchi yake, Misri, na ametoa huduma
nyingi kwa michezo ya kimisri na Misri
pia kwa viwango vyote, na leo ameheshimiwa kwa mafanikio yake kadhaa,
kile alichowasilisha na kile anachopeana kwa Misri yetu, na leo ni siku ya kutimiza Leo ni siku ya
uaminifu kwa mkubwa na baba wa kiroho wa
michezo ya kimisri.
Kwa upande wake, Hisham Nasr, Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Mikono, alisema ninafurahi na ni heshima ya kuwa katika mchezo unaotokana na
mhusika mkubwa kama vile Dokta Hassan Mustafa, kwa kuwa yeye ni mhamisishaji
mkubwa wa michezo ya kimisri kwa jumla na mpira wa mikono, na kila wakati
anaongeza uzoefu na ushauri wake mwingi kukuza michezo ya mpira wa mikono.
Comments