Mnamo sherehe ya siku ya Afrika.... Waziri wa vijana na Naibu wa baraza la wawakilishi wanaheshima washindi wa mashindano ya "Waanzishi wa Umoja wa kiafrika
- 2019-05-27 20:06:43
Dokta Ashraf Sobhy -Waziri wa vijana na michezo - na Bwana Mahmoud
Elsharif -Naibu wa kwanza wa Bunge-
waliheshima vijana waafrika washindi katika mashindano ya kiufundi kwa kutekleza
picha ya kisanaa kwa baba mmoja wa waanzishi wa Umoja wa kiafrika, na cheo cha
kwanza kilipatwa na Idres Zarif toka nchi ya Morocco, na cheo cha pili kwa
Muhamed Said Elmansy toka nchi ya Misri, na cheo cha tatu kilikuwa kwa Abidun
Ogonfudu toka nchi ya Nigeria.
Na hayo yote yalitokea kupitia sherehe ya Wizara ya vijana na michezo
juu ya jukwaa la kiroma, katika kituo cha vijana wa Aljazira, kusheherekea siku
ya Afrika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya 56 kwa uanzishi wa shirikisho la Umoja
wa kiafrika (Umoja wa kiafrika hivi
sasa), kwa mahudhurio ya mshauri Ahmed Saad Eldin - karibu mkuu kwa Bunge -, na
Mwakilishi Mai Mahmoud -mwanachama wa tume ya mambo ya kiafrika na Bunge la
kiafrika, Balozi Muhamed Nasr Eldin - Rais wa jumuiko la kiafrika-, na idadi
kadhaa toka mabalozi na wakilishi wa balozi za kiafrika hapa nchini Misri.
Na mnamo kauli yake, Waziri wa vijana na michezo alisema : " leo
tunakutana kwa ajili ya kusherehekea kumbukumbu adhimu sote tunaiheshima,
kumbukumbu ya uanzishi wa shirikisho linalojumuisha nchi za kiafrika nalo ni
Umoja wa kiafrika, na tunahisi fahari kwa sherehe hii kwani inatokea sawa sawa
na urais wa Misri chini ya uongozi wa rais Abd Elfatah Elsisi kwa Umoja wa
kiafrika. "
Aliendelea: " nafurahi sana kwa mikutano wa vijana wa kiafrika, na
shime yao ya kupatikana hapa ili kusherehekea siku hii, basi shsherehe hii
inatoa mwanga juu ya tofauti inayojaa barani katika sekta zote, na kuangalia
Vipaji vya vijana wa bara la Afrika.
"
Na matukio ya sherehe yalikusanya sehemu ya kisanaa kwa ushirikiano wa Bendi
ya Wizara ya vijana na michezo kwa uongozi wa Maistru Karim Zain nayo ni kama
" This time for Afrika", kwa amani tulianza kwa amani, ipende nchi
yako kama inayopo, Misri itazidisha kheri na nuru kwa kuwepo kwenu, "This
is me", Afrika the cup of life, picha kubwa sana kwa sanaa za kiurithi za
kiafrika( wanafunzi wa chuo kikuu cha Ain shams, vijana wa kusini mwa Sudan, Kenya,
Kongo, Sudan, Mali), na maonyesho ya nguo za kijadi kwa nchi kadhaa za kiafrika.
Inatajwa kwamba wajumbe waafrika walioshiriki
katika sherehe hii wapo kutokana nchi za Ghenya Bissau, Mamlaka ya kimorocco,
Algeria, Ghana, Uganda, Madagascar, Mauritania, Zimbabwe, Kenya, Kongo
Demokrasia, Kameron, Côte d'Ivoire , Somalia, Iritria, Gabon, Benin, Nigeria,
Tanzania, Kusini mwa Sudan, pamoja na Misri.
Comments