Waziri wa Vijana na Michezo na Waziri wa Mshikamano wa kijamii huwaheshimu mama bora
- 2020-03-09 11:51:43
Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, na Nevine El Kabbaj, Waziri wa Mshikamano wa kijamii, waliheshimu idadi kutoka mama bora katika sherehe kuu iliyofanyika katika Kituo cha Vijana cha Shahidi Sherif El-Sebaei Abdel Sadiq, "Kituo cha Vijana cha Kairo mpya" kwenye Eltagamoa Elkhames.
Sherehe hiyo
ilihudhuriwa na kikundi cha familia za Kairo mpya, wanachama wa kituo ,idadi ya viongozi wa
wizara za vijana na michezo na mshikamano wa kijamii, baraza la wakurugenzi wa
kituo , idadi ya maafisa kadhaa wa wakurugenzi wa elimu huko Kairo na Giza, wakilishi wa taasisi za sekta
binafsi, Hani Aziz, Katibu Mkuu wa Chama cha wapendwa wa Misri ya Amani,
msanii Rajaa El-Jeddawi, Na
msanii Wafa Amer.
Maadhimisho
yalikuja pamoja na wimbo, kuheshimu
kikundi cha mama wa mashahidi wa nchi hiyo, na vile vile kuwaheshimu mama bora
huku pamoja na kuwepo kukubwa kwa watoto wa Kairo mpya.
Katika hotuba yake,
Waziri wa Vijana na Michezo alionyesha furaha yake kwa kukaribisha Kituo cha Vijana cha shahidi Sharif Al-Sebaei
Abdul Sadiq kwa sherehe ya kuwaheshimu mama bora katika sherehe ya Siku ya
Mama, akizungumzia jukumu muhimu la vituo vya vijana wa Misri ambao huzingatiwa
toka serikali ya kimisri, na Wizara ya
Vijana na Michezo inaendeleza na kuboresha jukumu lake. Ndani ya jamii.
Dokta Ashraf Sobhy
aliwashukuru washiriki wote katika maadhimisho hayo, na kuwepo kukubwa
kwa familia za kimisri kwa njia ya shukrani za dhati na kuthamini jukumu la
mama.
Kwa upande wake,
Waziri wa Mshikamano wa kijamii alishukuru
kila mama mmisri anayelea watoto wake, na kueleza kuwa Wizara inatoa
msaada wote kwa mama wa Misri katika mikoa yote kupitia programu kadhaa, na
mnamo kipindi kijacho itaelekea kwenye uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake,
shukrani kwa jamii zinazoshiriki na Wizara katika kuvutia shughuli za kijamii.
Comments