El-Fouly, ni mkurugenzi wa kamati la watu mashuhuri katika Shirikisho la kimataifa kwa Taikondo
- 2020-03-09 12:01:29
Shirikisho la kimataifa kwa Taikondo kwa uongozi wa Chung Wan Shu, alichugua
Jenerali Ahmed El-Fouly awe mkurugenzi wa Shirikisho la Afrika na makamu wa kwanza
wa mkurugenzi wa Shirikisho la kimataifa, pia Mkurugenzi wa kamati la ukumbi wa
watu mashuhuri wa Taikondo ya dunia.
Na Jenerali El-Fouly amechuguliwa kama mkurugenzi wa kamati,
kwani yeye alikuwa katibu wa kwanza wa mkurugenzi wa Shirikisho la
kimataifa basi yeye ni katibu mkale zaidi kwa mkuu. Kama kwamba jukumu la kamati ni kuchugua
wagombea kwa ukumbi wa watu mashuhuri na pia kutoa mabadiliko kuhusu sharia za
kila mwaka.
Dokta. Chu, mkurugenzi wa Shirikisho la kimataifa kwa
Taikondo , akapeleka barua ya kuidhinisha kwa jenerali Ahmed El-Fouly, na
ilikuja katika barua hii : “kama
nilivyotangaza katika mkutano wa muda wa
Jumuiya kuu uliofanyika mjini Moscow mnamo mwezi wa Desemba iliyopita, kuwa nataka kutangaza wagombea wa kwanza
wakati wa mkutano ujao uliopangwa kufanyika Mei 12 mjini Lausanne, ili tuweze
kualika na kuheshimu wagombea hawa mnamo Oktoba ujao , mjini Sofia, pembezoni
mwa Mashindano ya Ulimwengu kwa Vijana,
na kwa suala hilo ushiriki wako katika kuchagua wagombea kwa ukumbi wa
watu mashuhuri ni muhimu sana. Nami nakushukuru sana, na nakutakia mafanikio katika madaraka mapya
hayo”.
Na mkurugenzi wa Teikondo ya ulimwengu anategemea sana
jenerali Ahmed El-Fouly, kwani yeye akahakikisha mafanikio ya ajabu sana katika
Taikondo ya kiafrika, mnamo urais wake kwa Umoja wa Afrika , ambapo
idadi ya nchi wanachama zinazoshiriki
katika Jumuyia kuu ni nchi 52. Pia wachezaji kadhaa wa bara la Afrika wakawa
wenye medali za kidunia na Olimpiki.
Na (Mkuu wa Teikondo ) alikuwa akipewa Shirikisho la Afrika
kwa uongozi wa Jenerali Ahmed El-Fouly uandaaji wa mashindano ya Kombe la Rais
mwezi wa Desemba ujao, mjini Aswan huko Misri . Na hivyo baada ya Cote d'Ivoire
ilijiondoa kutoka uandaaji wa mashindano hiyo. Na jenerali Ahmed El-Fouly anafanya bidii yake kubwa, ili kuandaa mashindano ya kidunia yanayofaa jina la
Misri, hasa baada ya Morocco iliandaa matoleo mawili ya kwanza ya mashindano
hiyo kwa mafanikio makubwa sana .
Comments