Waziri wa vijana na michezo anafungua klabu ya ( Al-Nady ) katika eneo la Oktoba 6

 

Dokta Ashraf Sobhy  Waziri wa vijana na michezo amefungua klabu mpya katika eneo la  Oktoba 6 baada ya kuandaa na kumaliza kazi ndani yake.

 

Mshauri ( Alaa Fouad )  Waziri wa Halmashauri na Dokta ( Al Sayed Alkosyer )  Waziri wa Kilimo wamekuwepo na Waziri wa vijana na michezo, ufunguzi umejumuisha baadhi ya vipindi vya kuimba, pamoja na ziara ndani ya klabu ili kukagua majengo yake mbalimbali yaliyokusanya jengo la Boga, jengo la kiafya na la kijamii, sebule ya sarakasi na bwawa la kuogelea.

 

Klabu ya ( Al-Nady ) inajumuisha majengo mengi : nyanja za michezo 14, nyanja 4 kutoka nyanja hizo ni khomasi, pamoja na nyanja za michezo mbalimbali, pia nyanja 6 kwa michezo mbalimbali za kupambana, sebule ya sarakasi na Boga,  mkusanyiko wa mabwawa ya kuogelea unajumuisha bwawa la kuogelea la Olimpiki, na eneo la huduma linajumuisha tawi moja la benki.

 

Ufunguzi wa klabu ya ( Al-Nady ) unakuja mnamo wakati wa kujali kwa wizara ya vijana na michezo kwa vijana na wavulana kutoka wachezaji wa michezo mbalimbali ili kuandaa kizazi kipya kinachoweza kuifikisha Misri kwa nafasi bora zaidi za kimataifa katika michezo zote.

 

Ashraf Sobhy amesema kuwa mradi wa klabu ya ( Al-Nady ) unazingatia kutoka miradi mikubwa ya kimichezo inayotoa huduma zote za kimichezo kwa vijana na familia ya kimisri, kwa sababu ya majengo yake ya kipekee yanayotoa huduma kwa michezo zote za riadha, akiashiria kuwa wizara inatia mpango kamili ili kufanya kazi mlolongo wa mradi wa klabu ya ( Al-Nady ) kwa ushirikiano na sekta ya kibinafsi.

 

Inabidi kutaja kuwa Dokta Ashraf Sobhy  Waziri wa vijana na michezo ameshuhudia kusaini kwa itifaki 3 za ushirikiano kati ya baraza la waamini wa mlolongo wa klabu ya (Al-Nady) na benki tatu za (benki ya mfereji wa Suez), (benki ya uwekezaji wa kiarabu) na (benki ya majengo  ya  kimisri ya kiarabu), ili kufadhili uwanachama moya za klabu.

 

Kwa mujibu wa protokoli za ushirikiano, benki hizo zinafadhili uwanachama mpya katika klabu ya (Al-Nady), tawi la Oktoba 6, hii katika mfumo wa kujaribu kwa klabu kuuza uwanachama ili kutoa huduma za kimichezo na kijamii, pamoja na shughuli zingine za kimichezo zinazopatikana ili kuhakikisha malengo yake.

 

Itifaki hii inakuja ili kusisitizia ushirikiano kati wizara ya vijana na michezo na taasisi kubwa za kiuchumi ikiwemo benki za Kimisri ambazo zinatoa programu za kufadhili kwa usajili kwa idadi ya klabu za michezo pamoja na kufadhili kwa watu wanaotaka usajili katika mradi wa (Al-Nady) baada ya kutimiza masharti yanayohusiana na kila  benki.

 

Waziri ametoa shukrani kwa maafisa wa benki za Kimisri juu ya kufadhili usajili za uwanachama za wanachama wa klabu, akiashiria kuwa wizara inakusudia kupanua katika matawi ya klabu ya (Al-Nady) mnamo kipindi cha miaka miwili kwa kufungua matawi mawili mapya, tawi moja litakuwa katika kituo cha maendeleo ya kimichezo katika eneo la (Sheraton, Misri AlGadida), na tawi jingine litakuwa katika mji mkuu mpya wa kiutawala.

 

Wanachama wa baraza la uongozi wa klabu ya (Al-Nady), Dokta Ehab Amin  mwenyekiti wa shirikisho la sarakasi Ia Kimisri na mwanachama wa Kamati ya Olimpiki na maafisa wa wizara ya vijana na michezo wamehudhuria sherehe hiyo.

Comments