Kwa Uongozi wa Dokta Ashraf Sobhy, Ofisi ya vijana wa kiafrika inashiriki katika kuonyesha shughuli za Wizara ya Vijana na Michezo kwa Kamati ya masuala ya kiafrika kwenye Halmashauri
- 2020-03-11 22:03:26
Kamati ya Masuala ya kiafrika na idadi ya wakilishi wa kamati maalum katika Bunge la kimisri linaloongozwa na Mwakilishi Tarek Radwan walikutana na timu ya Wizara ya Vijana na Michezo kwa mahudhurio ya Waziri Dokta Ashraf Sobhy na viongozi kadhaa wa mawaziri kwa ajili ya kuonyesha shughuli za Wizara ya Vijana na Michezo katika uwanja wa Kiafrika.
Ofisi ya Vijana ya Kiafrika ilionyesha shughuli zake mnamo kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi sasa, mnamo kipindi kilichoambatana na urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika, inayopasa kutajwa ni kwamba shughuli za ofisi hiyo zinaambatana na Ajenda ya Afrika 2063 na malengo ya maendeleo endelevu.
Timu ya Wizara hiyo imesifiwa kutoka kwa wanachama wa Halmashauri kwa juhudi kubwa iliyotolewa kwa Wizara wakati wa Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika
Comments