Sauti kutoka Afrika .. matoleo ya hivi karibuni ya mamlaka ya katibu

 Hivi karibuni,  Mamlaka kuu  ya  kimisri kwa kitabu,  kinachoongozwa na Dokta Haitham Al-Haj Ali,  ilitoa kitabu  kwa kichwa cha   "Sauti kutoka Afrika - Daraja kuelekea Ubunifu wa Bara la Afrika  ", kilitungwa na kikundi cha wabunifu waafrika, kilitafsiriwa na kuwasilishwa na Nasr Abd El  Rahman.


 Kitabu hiki kinaangazia  baadhi ya sifa za fasihi ya kiafrika na waanzilishi wake mashuhuri wanaume na wanawake  katika awamu tofauti.  Pia inaangazia umuhimu wa ushairi wa mdomo kama moja wapo ya mhimili muhimu wa ubunifu wa kiafrika na kuangalia sifa za upekee wake ulimwenguni.


 Pia kinaangalia mabadiliko ya kisiasa na ya kijamii kati ya zamani na sasa, na kiasi cha kuathiri kwake juu ya mtindo wa kifasihi kwa sasa, kama inaonyesha ushawishi wa kiutamaduni wa magharibi katika ubunifu wa wana wa bara la Afrika,  sawa ikiwa mnami zamani au  sasa, na kinaashiria jukumu la taasisi za kiutamaduni za kimaeekani na kiulaya katika kusaidia au kuwaongoza wabunifu wa vizazi vipya, na athari ya hivyo juu ya njia yao ya kushughulika kwa masuala tofauti.


 Kitabu hiki kinazingatia  kutoa majaribio mengi kwa wabunifu wanaume na  wanawake kutoka kwa vijana wa bara hili mnamo wakati wa kisasa  lli kujua kiwango cha maendeleo ya fasihi ya Kiafrika na mielekeo yake kwa suala la ubunifu na kutarajia mustakbali yake mnamo miaka michache ijayo. 

Comments