Hirizi ya michuano ya mataifa ya kiafrika: toka mwaka wa 2006 hadi mwaka wa 2019, vipi Hirizi ya kombe la mataifa ya Afrika iliendelea?
- 2019-05-28 13:55:51
Kamati iandaayo
imetangaza Hirizi ya michuano ya mataifa ya kiafrika2019 , na hii ni Michuano
inayopkewa kwa mara ya kwanza kwa Misri tangu mwaka 2006, na itaanza tarehe 21,
mwezi wa sita hadi tarehe 19, mwezi wa saba ujao.
Kwa kweli, uundaji
wa Hirizi ya michuano ya Afrika , ilikuwa kama
mtoto mmisri mwenye umri wa miaka 12, akivaa shati ya timu ya Misri pamoja na mavazi ya
kifarao, aliitwa kwa jina la
"TUT" kwa kamati iandaayo michuano ya kiafrika nchini Misri, ili
kuenda na historia ya kifarao .
Pia, kamati
hiyo iandaayo michuano ya mataifa ya
Afrika 2019 imechapisha kielelezo cha TUT, kinachotoa taarifa kadhaa kuhusu
Hirizi ya TUT, kwa lugha tatu. Nazo ni
Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa.
Kielelezo hicho kimekuja baada ya kutangaza Hirizi ya TUT kwa njia
rasmi.
Kielelezo hicho
kimeeleza kwa ufupi kuwa TUT ni mtoto mmisri mwenye umri wa miaka 12, na anapenda
sana kandanda, katika jaribio la kuunganisha vijana na michuano ya mataifa ya
Afrika itakayofanyika mwaka 2019 nchini Misri.
Aidha, Hirizi mpya
hiyo imeshuhudia maswali na maoni kadhaa kutoka kwa wananchi wa Misri
ambapo wapo watu waliounga mkono hatua hii na mabadiliko hayo ya Hirizi , huku
wengine walikataa mabadiiliko mapya haya
ya Hirizi. Lakini mara hii idadi ya
waliounga mkono mabadiliko hayo ya Hirizi ilishinda wale waliokataa.
Hirizi ya mwaka wa 2006 ilikuwaje kwa michuano ya mataifa ya
Afrika 2019?
Tukirudia nyuma
kidogo (mwaka 2006), tutatambua kuwa kamati
iandaayo michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2006 imewahi kufanya
sherehe kubwa ndani ya ikulu (Jumba ) ya Muhammed Ali iliyoko mtaa wa El-Maniel
ili kutangaza Hirizi ya michuano 2006.
Hii ilikuja katika kipindi cha uongozi wa Hani Abu Riida, aliyekuwa
kiongozi wa Shirikisho la Soka la kamati
iandaayo michuano wakati huu.ِِ
Comments