Sherehe nzuri ya ufunguzi kwa Mashindano ya Kiafrika kwa Sarakasi na Aerobiki mjini Sharm El-Sheikh
- 2020-03-15 14:33:53
Jioni Alhamisi, Shughuli za Mashindano ya 15 ya Kiafrika kwa Sarakasi na Aerobiki zilianzishwa, yaliyokaribishwa na Misri mnamo kipindi cha 10 hadi 17 Machi mwaka huu, katika ukumbi uliofunikwa mjini Sharm El Sheikh kwa ushiriki wa wachezaji 110 wa wavulana na wa wasichana kutoka nchi 12, ambazo ni Misri, " nchi mwenyeji ", Tunisia, Algeria, Morocco, Afrika Kusini, Cape Verde, Senegal na Congo Angola, Namibia, Zimbabwe na Benin.
Sherehe ya ufunguzi ilianza na foleni ya maonyesho kwa nchi zinazoshiriki, kwa mahudhurio ya Dokta Ehab Amin, Rais wa Shirikisho la kimisri kwa Sarakasi ,na mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kamati ya Olimpiki, na wanachama wa Shirikisho na wajumbe wa nchi zinazoshiriki.
Sherehe ya ufunguzi pia ilishuhudia kuwepo kukubwa kwa mashabiki walioingiliana na maonyesho ya kisanii ya wachezaji hao, ambapo timu ya Misri ilishinda sehemu kubwa zaidi ya kuhimiza.
Mashindano hayo yatafanyika kwa awamu mbili, ya kwanza kwa Sarakasi kutoka 10 hadi 14 Machi, inayofikisha michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020, ambapo timu inayoshinda lakabu inashiriki kwenye Olimpiki.
Na timu ya kitaifa kwa Sarakasi kwa wasichana , Chini ya uongozi wa mtaalam wa kimataifa wa Urusi Natalia Dimitrova, inahangaika kupata kadi ya kufikia .
Awamu ya pili ni mashindano ya michuano yanayohusiana na Sarakasi ya Aerobiki kutoka 13 hadi 17 Machi.
Kwa upande wake, Dokta Ehab Amin, Rais wa Shirikisho la kimisri kwa Sarakasi na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kamati ya Olimpiki, alisisitiza kwamba mashindano hayo ni ya kushiriki zaidi na wachezaji na nchi katika kiwango cha mashindano ya kiafrika.
Shirikisho hilo lilitunza kufanyika mashindano katika Sharm El Sheikh kwa mara ya kwanza ndani ya mpango wa shirikisho la kueneza mchezo katika mikoa yote na kuhimiza Utalii wa kimisri.
Comments