Kamati ya Olimpiki inapongeza timu ya kitaifa ya Sarakasi kwa kufikia michezo ya Olimpiki ya Tokyo baada ya kushinda medali ya kidhahabu ya Afrika

Kamati ya Olimpiki chini ya uongozi wa Mhandisi Hisham Hatab imelipongeza shirikisho la Kimisri kwa sarakasi na timu ya kitaifa ya Sarakasi  inayoongozwa na kocha Mrusi ( Natalie Demetrova ) kwa kufikia fainali za kikao kijacho cha michezo ya Olimpiki, kilichopangwa kukifanyika katika mji mkuu wa Japan, Tokyo.


Wasichana wa ( Mafarao ) wamefikia michezo ya Olimpiki baada ya kupatia medali ya kidhahabu katika michuano ya kiafrika inayokaribishwa mjini mwa Sharm El sheikh mnamo kipindi cha tarehe 10 hadi 17 Machi.

Imetajwa kuwa timu yetu ya kitaifa imeshinda nafasi ya kwanza kwa medali ya kidhahabu baada ya kupata pointi 23,4.


Huku timu ya kitaifa ya Afrika Kusini imechukua nafasi ya pili, lakini timu ya kitaifa ya Algeria imechukua nafasi ya tatu.


Dokta Ehab Amin amesisitiza kuwa tija ile ni mabadiliko makubwa na ya kipekee kwa timu yetu ya kitaifa, hasa baada ya mazoezi ya kipekee chini ya usimamizi wa kocha Mrusi.


Amin ameongeza kusema kuwa ataendelea katika uandaaji wa timu ya kitaifa mpaka inaweza kushindana katika michezo ya Olimpiki ijayo, hasa kuwa sisi tumekaribia kuhakikisha rekodi inayohusu mashindano juu ya kuingia miongoni mwa timu 8 bora zaidi ulimwenguni, rekodi hiyo ni pointi 25.


Comments