Al-shamy : waziri wa vijana na michezo mwungaji mkono mkubwa kwa mapokezi ya Misri kwa michuano ya dunia kwa mchezo wa ujenzi wa mwili

Mhasibu Ahmed Al-shamy  naibu mwenyekiti wa shirikisho la Kimisri kwa uzima wa mwili ametangazia  mambo yaliyo nyuma ya mkutano wa Dokta Rafail  Santonga  mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa pamoja na Dokta Ashraf Sobhy  Waziri wa vijana na michezo, kwa mahudhurio ya Dokta Adel Fahim  mwenyekiti wa shirikisho la Kimisri Ia ujenzi wa mwili, pamoja na mwenyekiti wa mashirikisho mawili ya kiarabu na ya Kiafrika, pia naibu mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa, na mkutano huo umeshuhudia majadiliano kuhusu masuala muhimu mbalimbali kati ya pande mbili zote, jambo lililokuwa muhimu zaidi ni uwezekano wa kukaribisha Misri kwa michuano ya dunia kwa ujenzi wa mwili iliyopangwa  kufanyika mwezi wa Novemba ujao , kwa sharti kwamba Uchina inatoa msamaha rasmi kwa kutokaribisha, na kuwa michuano hiyo itakuwa chini ya uangalifu wa mheshemiwa rais Abd El Fatah  Elsisi, na pia misaada yote itatolewa kwa ajili ya mafanikio ya michuano  hiyo, na kuwa na mimenyuko ulimwenguni ili kuthibitisha kwa ulimwengu wote kuwa Misri ni nchi ya Usalama  na Amani .


Al-shamy ameeleza kuwa katika hali ya Uchina ikitoa msamaha rasmi, tutakuwa tayari ili kuandaa tukio la kimataifa kwa ushirikiano na Waziri wa vijana na michezo  anayeshirikiana na mashirikisho  yote ya kimichezo.


Naibu mwenyekiti wa shirikisho la Kimisri kwa ujenzi wa mwili ameashiria kuwa mazungumzo yamejumuusha kubadilisha ujenzi wa mwili mnamo kipindi kijacho, hii kwa kufanyika mazoezi mengi na mashindano yatakayorejea kwa manufaa kwa wachezaji wote wa mchezo wa Kimisri wa uzima wa mwili.


Naibu mwenyekiti wa shirikisho la Kimisri kwa ujenzi wa mwili ameongeza kusema kuwa Misri imeanza kupata tena nafasi yake ulimwenguni, hii kwa maamuzi ya utawala wa kisiasa, chini ya uongozi wa mheshemiwa Rais  Abd El fatah Elsisi,  aliyefanikiwa kuelekea kwa Misri kwenda Usalama  kwa mabadiliko katika nyanja mbalimbali kwa ujumla na michezo hasa, na mafanikio yaliyohakikishwa na mabingwa wetu katika michezo mbalimbali, na sisi kama shirikisho la ujenzi wa mwili tunamahidi kwa kuhakikisha mafanikio hayo hayo katika mashindano ya dunia mnamo kipindi kijacho, pia tutafurahi kwa kukaribisha Misri kwa michuano  ya dunia kwa uzima wa mwili mnamo mwezi wa Novemba ujao. 


Mwishoni mwa mkutano, Dokta Ashraf Sobhy na mgeni mkubwa wa Misri Dokta Rafael Santonga  mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa la michezo hiyo wamezibadilishana nishani. 


Comments