"Ushirikiano kati ya Wizara ya vijana na michezo na "Visa" kwa ajili ya kuwachagua watoto waambatanao wa wachezaji katika michuano ya mataifa ya Afrika".
- 2019-05-28 14:01:23
Kampuni ya
"Visa" kwa kushirikiana na Wizara ya vijana na michezo na Shirikisho
la "UNICEF" inatoa mpango kwa kuwachagua watoto toka pambe zote za
Jamhuri ili kuambatana na wachezaji kwenye michuano ya kombe la mataifa ya
kiafrika 2019.
Na matukio ya
programu hii yanatoa nafasi kwa watoto wa kiume na kike 47 toka umri wa miaka 6
hadi miaka 10 ili kushirikiana katika programu kupitia mikoa tofauti ya Misri
kama Kairo, Aleksandaria, Alesmailia, Asiuut, na Qena.
Na watoto wa
kiume na kike 47 kutoka Misri watapata nafasi ya kuambatana mchezaji mmoja na
kuongoza kundi la wachezaji bora zaidi duniani mnamo kuwepo kwao uwanjani, na
uchaguzi wa watoto hufanyikwa kulingana na mihimili mikuu tatu, wa muhimu zaidi
ni kuchagua washiriki 36 kutokana na michezo ya mpira wa miguu inayoandaliwa
kwa uangalifu wa Wizara ya vijana na michezo katika vituo vya vijana katika
pembe zote za Misri, pamoja na "Visa" na usaidizi wa shirikisho
la "UNICEF " iliandaa michezo
kwa watoto katika uwanja wa eneo la "Asmarat " ili kuchagua watoto 7
wengine kutokana na familia fukara zaidi, na eneo la Misri ya juu ili kupata
nafasi na kushirikiana katika programu, pamoja na kuwachagua watoto 4 wengine
wanaoshiriki katika kampeni ya "Visa" inayoitwa "Ndoto bila
mipaka" mnamo tovuti za mitandao ya kijamii.
Na kwa mnasaba
huu Dokta Ashraf Sobhy "Waziri wa vijana na michezo" alieleza kwa
kusema" Riadha ni njia moja kuu ili kuunganisha watu kutokana pande zote
za dunia, ambapo inawajumuisha watu wanaoonyesha upendo na hamasa tu kwa jambo
binafsi, na kwa sababu hiyo na sababu ya kukaribisha Misri kwa michuano mikubwa
zaidi ya mpira wa miguu duniani,
hatukuwa na budi ila kushirikiana ili kutoa nafasi ya kushirikiana katika
programu hii kwa tunaodhani wanastahiki".
Kwa upande
mwengine Bwana Ahmed Gaber" Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Visa kwenye
kaskazini ya Afrika" alisema kwamba tunahisi fahari adhimu kwa kuwa
wachungaji wakuu kwa michuano mikubwa ya tatu juu ya Sayari , nayo ni michuano ya kombe la mataifa ya
kiafrika Total 2019 basi wamisri ni wananchi wenye harakati, upendo, na
matarajio zaidi duniani, na hilo linaloelezea sababu yetu "Visa" ya
kutia mwanga juu ya upendo na hamasa yao isiyo na mipaka , kwa jambo hilo
linatoa kampeni yetu "Visa bila mipaka" ili kuonyesha visa vyenye
shauku zaidi kutokana na mitazamo ya vijana wetu mnamo ushirikiano wao na Dunia.
Bwana Porno
Mars" Mwakilishi wa shirikisho la "UNICEF "alieleza kwa kusema
" michezo ya mtaa wa "Al Asmarat " inazingatiwa mpango adhimu
kutokana na Wizara ya vijana na michezo na kampuni ya "Visa", pia tuna furaha kubwa kwa usaidizi wa
"UNICEF " kwa watoto, khasa eneo la Misri ya juu ili kupata nafasi ya
kushirikiana katika muda nzuri hii ya nyakati za mpira wa miguu.
Akiongeza
kwamba" sisi katika "UNICEF" tunathamini umuhimu wa kuwepo
kukubwa kwa baba pamoja na wana wao, wanawashirikiana kucheza na nyakati za
furaha kama kutazama pamoja mchezo mzuri.
Inapaswa kutajwa
pia ni kwamba harakati za "Visa" hazipatikani katika kuunda michezo
ya mpira ili kuwachagua watoto washiriki tu,
bali kampuni itatoa kampeni kwenye mitandao ya kijamii pamoja na mtangazaji
maarufu wa programu za kimichezo
"Saif Zaher" na mtangazaji maarufu wa Redio"Khaled Elesh"
ili kuhamasisha watafutaji wao kwa kusaidia watoto kupitia kushiriki video
ambapo watoto wanasimulia kisa fulani chenye mafanikio, au mtu bora linalochangia
kufuata ndoto zao kupitia Hachtag ya #UnstoppableStories, na video nne zenye
utazamaji na uangalifu zaidi zitapata nafasi ya kushirikiana katika programu ya
kuambatana wachezaji, kampeni inalenga kuonyesha visa vyenye faida na visivyo
na mipaka nichini Misri, linalotengeneza njia mbele ya vijana wetu ili
kunufaisha toka kwake.
Comments