Waziri wa Michezo ajadili pamoja na Wizara za Mambo ya nje, ndege ya umma na Afya kuhusu taratibu za kurudisha wachezaji wa Misri kutoka nje

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana, aliratibu na vyombo tofauti vilivyohusika, hasa Wizara ya Mambo ya nje ya kimisri na Wizara ya ndege ya umma, pamoja na uratibu unaoendelea na Mhandisi Yasser Idris mjumbe wa Kamati ya Olimpiki ya kimisri, kufafanua orodha ya majina ya wachezaji walio nje ya Misri ambao walikuwa wakishiriki katika mashindano mengi na makambi ya nje.



Hii inakuja kwa kuzingatia maagizo ya Rais wa Jamhuri na maamuzi ya bwana Mhandisi Waziri Mkuu kuhusu uratibu uliochukuliwa kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Corona, na uliohusiana  kwa kukomesha ndege ya kimataifa, na katika mraba wa kufuata hali ya wachezaji wamisri ambao wako nje ya nchi na ambao hawawezi kurudi Misri kwa sababu ya kusimamishwa kwa ndege.



Dokta Ashraf Sobhy amesisitiza kuwa uratibu umefanywa na vyombo mbali mbali vinavyohusika kuhusu kuchukua hatua za kuwarudisha wachezaji waliopo katika nchi tofauti za ulimwengu na kulingana na mahitaji na uwezekano wa ndege za kuwarudisha haraka iwezekanavyo.



Akionyesha kwamba Wizara ya Vijana na Michezo inaenda sambamba na  maamuzi ya Baraza la Mawaziri yanayotoka kwa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya kufuata kikamilifu hali ya Wamisri wote walio nje ya nchi, pamoja na wachezaji ambao walikuwepo kushiriki katika makambi na mashindano ya nje na kurudi kwao hakuwezekani kwa sababu ya hatua za kimataifa za kukomesha ndege ya kimataifa.



Waziri wa Michezo alieleza kwamba uratibu unafanyika sambamba na wizara ya mambo ya nje, ndege ya umma na afya kufuata kukamilika kwa taratibu zote, hasa kuhusu miadi za kuwasili kwa wachezaji, kuchukua hatua zote za kiafya na  kuhusu kurudi kwa Wamisri kutoka nje ya nchi, kuhakikisha usalama wao ikiwa watarejea nchini.

Comments