Mwakilishi wa shirika la afya ya Dunia: Wafanyikazi wa matibabu nchini Misri wanatia juhudi zao zote kwa ajili ya kuokoa roho
- 2020-03-31 12:27:07
John jabour mwakilishi wa shirika la afya ya Dunia mjini Kairo aliwashukuru madaktari na wafanyikazi wauguzi na wafanyikazi wengine katika uwanja wa afya, wanaofanya kazi ya kupambana na janga hili, wanafanya kila juhudi kuokoa roho,chini ya uongozi wa Dokta Hala Zaid waziri wa afya na makazi.
Alisema kuwa tunahitaji kujitolea kutoka serikali, sekta ya afya na jamii sawa kupambana na janga hili na hii inahitaji kiwango cha juu cha uratibu na ushirikiano, iwe ni katika ngazi ya serikali au kati ya raia na serikali, sote tunahusika na suala hilo, na kila mmoja wetu ana jukumu la kuchangia, na lazima sote tunashikamana pamoja, Hatupaswi kuruhusu hofu kutushinda katika vita vyetu na virusi hivi, na lazima pia tujifunze kutoka kwa uzoefu wa nchi ambazo ugonjwa umeenea na kusaidia kupunguza kuenea kwa jamii.
Ujumbe wangu hapa kwa jamii ya kimisri ni: kila mtu anapaswa kukaa nyumbani mwake ili tusiweke shinikizo kwenye mfumo wa afya, kwamba wanafuata njia zote za kuzuia, na hutunza afya zao za mwili na kiakili . Mbakishe katika Amani na Afya.
Comments