Misri inakusanya juhudi ili kuunda mpango wa kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na athari za janga la virusi vya Corona
- 2020-03-31 12:31:44
Katika mfumo wa juhudi kamili za Kimisri ili kukabiliana na shida ya virusi vipya vya Corona, Balozi Mohamed Edres, mjumbe wa kudumu wa Misri katika umoja wa mataifa mjini New York amefanya mashauri pamoja na maafisa wa shirika la kimataifa ili kukusanya na kuangalia juhudi kwa ajili ya kuunda mpango wa kimataifa wa kukabiliana athari za janga la virusi vya Corona kwenye viwango vyote vya Afya, kiuchumi na kijamii.
Balozi Mohamed Edres ameeleza kuwa ujumbe wa kudumu wa Misri huko Umoja wa mataifa mnamo tarehe 29/3/2020 umepeleka barua kwa mwenyekiti wa kundi la 77 na China na ujumbe wote wa mataifa wanachama wa umoja wa mataifa, unajumuisha idadi kadhaa ya mambo na kanuni za kimisingi ambapo Misri inaona kuwa inawezekana inachangia kuweka maoni ya kimataifa na mpango kamili kwa umoja wa mataifa kuhusu changamoto za kimataifa za kisasa mnamo muda mfupi na mrefu, pia barua hii inasisitiza umuhimu wa kuwa mpango kamili inazingatia mambo mengi ya shida za kimataifa, na uratibu unafanywa kuhusu yake kati ya pande zote, pamoja na dharura ya kuhamasisha kwa rasilimali na uratibu wa juhudi kati ya umoja wa mataifa na shirika la Afya ulimwenguni pamoja na mashirika mengine ya kimataifa ili kukabiliana na athari za kibinadamu zinazotokana na maradhi, na umuhimu wa ushirikiano wa jamii ya kimataifa mnamo wakati huu unaozingatia changamoto kwa mamlaka za kimataifa za kisasa na uwezo wake wa kuhakikisha malengo na matarajio ya mataifa na wananchi kuhakikisha maendeleo endelevu na kurejesha Amani na Usalama katika maeneo mbalimbali duniani.
Mjumbe wa kudumu wa Misri ameongeza akisema kuwa mpango wowote wa Umoja wa mataifa, awali ni muhimu unajumuisha kuchukua hatua tatu za dharura na za kimsingi, zikiwamo ushirikiano ili kukuza chanjo na matibabu kwa janga la virusi ya Corona pamoja na kuzikidhi kwa mataifa yote ya wanachama Bila ya ukiritimba au tofauti , na orodha ya kimataifa inajumuisha mahitaji ya haraka ya vifaa na dutu za dawa vinavyohitajika kwa mataifa mbalimbali ili kukabiliana na maradhi na kampuni za wasambazaji kwenye ngazi zote za kimataifa na kuwezesha ufikiaji kwa mataifa , ukiongezea na umoja wa mataifa unafanya uratibu pamoja na benki ya dunia na mfuko wa fedha wa kimataifa ili kuweka mpango wa uungaji mkono wa kiuchumi kwa mataifa mataifa zinazoathiriwa na athari mbaya za kiuchumi zinazotokana na maradhi, akiashiria kuwa Misri inahangaika kufanya uratibu na Sekretarieti ya Umoja wa mataifa na nchi zingine ili kuunda mpango uliopendekezwa na kuutekeleza kwa upesi.
Comments