Hassan Mustafa: Hakuna nia ya kuahirisha Kombe la Dunia kwa mpira wa mikono

Dokta Hassan Mustafa, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mikono wa Kimataifa na mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, alithibitisha kwamba anapigania kwa nguvu zote ili asiahirishe Mashindano ya Dunia ya Mpira wa mikono,  yanayopangwa kufanywa nchini Misri Januari ijayo.



Mustafa alifafanua, katika taarifa yake, kwamba mawasiliano na mazungumzo na viongozi wa michezo ulimwenguni kote hayatatatizwa, yakiongozwa na Mjerumani Thomas Bach, Rais wa Kamati ya Olimpiki ya kimataifa, na kuongeza kuwa alimuuliza atunze mashindano makubwa ya michezo ulimwenguni bila ya  kubadilisha tarehe, hasa  baada ya Olimpiki kuahirishwa, Ratiba ya ulimwengu inashughulisha zaidi mnamo mwaka ujao.


Mustafa alisisitiza kwamba, hadi sasa, anafuata kushikilia michuano kwa wakati, isipokuwa kama Misri ikiomba kuchelewesha kwa sababu ya kusimamishwa kwa harakati za kazi katika viwanja vilivyopangwa kukaliwa na Kombe la Dunia.


Alisema kuwa maoni hayo yatakuwa wazi mnamo kipindi kitakachokuja ulimwenguni, na kwamba kila mtu anasubiri maamuzi ya Shirika la Afya Ulimwenguni, na kuongeza kuwa anafuata harakati ya janga la Corona saa kwa saa na kujadili maendeleo yote, akielezea furaha yake na idadi  ndogo ya kuenea kwa janga hilo nchini Misri ukilinganisha na Ulaya, ambayo inashambuliwa vikali.


Alionyesha kuwa kwa kufuata maandalizi ya Kombe la Dunia kabla ya kusimamishwa, ilikuwa inaendelea vizuri, lakini kuna uharibifu kadhaa kama matokeo ya kusimamishwa kwa muda na tunatamani  kutokuwa mrefu.


Kwenye kiwango cha kimataifa, alisema, hataweza kuchukua maamuzi yoyote madhubuti bila kurejelea Shirika la Afya Ulimwenguni na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, akiendelea " Mimi binafsi natamani mambo yaendelee kama kawaida na kutochukua uamuzi wowote wa dharura".

Comments