Aya Madany afichua taswira za kuahirisha Olimpiki ya Tokyo

Aya Madany, mjumbe wa Kamati ya wachezaji katika kamati ya olimpiki ya Kimataifa na Mwenyekiti wa kamati ya wachezaji kwenye shirikisho la Kimataifa kwa khomasi ya kisasa , alielezea kuridhishwa kwake kwa  kuainisha tarehe ya Olimpiki ya Tokyo,  iliyoahirishwa kwa sababu ya virusi vya Corona, mapema ambapo Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa ilitangaza kufanyika Olimpiki kutoka Julai 23 hadi Agosti 8, 2021.


Aya Madany alisema kuwa wachezaji wamisri wanapaswa kufaidika kwa kuahirisha Olimpiki kwa mwaka mmoja , kwa kuzingatia hali ya kisasa ambayo ulimwengu wote uliishi, ambapo wachezaji wengi wa ulimwengu wanajulikana kwa kuwepo kwa bustani ya kibinafsi ambapo wanaweza kufanya mazoezi wakati wa marufuku, na mabingwa wengi wa ulimwengu wana nafasi maalum ya mazoezi ndani ya nyumba zao, ambayo haipatikani na wachezaji wengi wa Misri. kwa hivyo Mabingwa wa Misri lazima wadumishe mazoezi ya mwili na kiufundi wakati wa kusimamisha mchezo ili waweze kurudi kwenye kiwango chao haraka iwezekanavyo.


"Madany" ameongeza kuwa kuahirisha Olimpiki kwa mwaka sio kwa maslahi ya wachezaji wengi. kwa sababu wachezaji wengi walijiandaa kikamilifu kabla ya kuzuka kwa  virusi vya Corona , kama kucheleweshwa hii kutaathiri mipango ya wachezaji kwa sababu Baadhi ya wachezaji waliahirisha masomo yake au ya ndoa yake au mambo yoyote ya kibinafsi ili kujitolea kuandaa olimpiki.


"Madany" alisisitiza kwamba uamuzi wa kuahirisha Olimpiki ilikuwa jambo la lazima kabisa, kwani afya ya wachezaji na kuwalinda kutokana na maambukizo ya virusi ya Corona ndio kipaumbele cha Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.


Na alifafanua kuwa uamuzi wa kuahirisha Olimpiki sio jambo rahisi, kwani kuna mambo mengi yanayohusiana na kikao cha michezo ya Olimpiki, ambayo lazima izingatiwe, ikiwa ni pamoja na maoni ya Kamati iandaayo ya Michezo na serikali ya Japan, mashirika ya kimataifa, ratiba ya mashindano ya kimataifa, wadhamini, na Kijiji cha Olimpiki kilichojengwa mahsusi kwa Michezo ya Olimpiki na kiliuzwa kwa watu ambao wangeimiliki baada ya Olimpiki kumalizika mnamo Agosti 2020.


Madany ameongeza kuwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa inafanya mkutano wa kila wiki na Kamati ya Wachezaji ili kujadili mambo yote na kufikia kuchagua maamuzi bora zaidi.


Siku ya Jumatatu, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki , Kamati ya Paralympiki,Kamati iandaayo kikao hicho, na Serikali ya Japan ilikubali kuzindua kikao cha Michezo ya Olimpiki mnamo Julai 23 na kufanya kikao cha Paralympiki kutoka Agosti 24 hadi Septemba 5, 2021.


Na alifafanua kuwa uamuzi huo ulichukuliwa kwa kuzingatia  mihimili mikuu mitatu nazo ni : kulinda afya ya wachezaji na kutoambukizwa kwa virusi vya Corona, kulinda haki za wachezaji na michezo ya Olimpiki na ratiba ya vyama vya kimataifa vya michezo ya Olimpiki.

Comments