Sura ya Heshima .. historia ya madaktari wa Misri pamoja na kupambana kuanzia daktari wa kwanza aliyekufa katika vita kama shahidi wa Corona
- 2020-04-02 22:31:03
Dokta Ahmed El-lawah ni daktari mmisri wa kwanza aliyekufa wakati wa vita vya virusi ya Corona ili kujiunga kwa orodha ya madaktari wa Misri wanaopambana , Maaskari wa safu ya kwanza wenye kanzu nyeupe
Wanaojitolea daima ili kuwaokoa wengine .na historia ya mapambano ya kimatibabu nchini Misri inajaza kwa picha za heshima na tunazieleza sehemu yake kwenu katika Mistari ifuatayo .
Historia ya Madaktari wa Misri pamoja na mapambano
Mohammed El-sayeh Adly ni Daktari shahidi wa kwanza vitani , Daktari mmisri wa kwanza aliyekufa katika silaha ya matibabu ya ufalme katika eneo la erq swedan , huko Ghaza katika vita vya palestina 1948
Shahidi Mohammed Elsayeh Adly ni kutoka Bani Helal , kituo cha Elmaragha , mkoa wa Sohag , alizaliwa katika siku ya pili mwezi wa Julai 1918 na babake alikuwa afisa wa polisi
Alijiunga kitivo cha Tiba na alipata Shahada ya kwanza katika mwezi wa Disemba 1941 na wizara ya afya ilimteua kama tabibu kisha alijiunga jeshi na alisisitiza kwenda kwa vita vya 1948 ili kupigania na alijenga hospitali ili kuwatibu waathirika wa vita
Naye ana misimamo kadhaa yenye ushujaa na Kujitolea kufanya kazi na miongoni mwake hospitali ya kuwatibu waathirika wa vita wakati ambapo afisa alipokuja kwake akiwa na majereha magumu katika wakati wa mashambulio ya adui na ilikuwa lazima wote waondoke eneo lakini yeye alisisitiza kufanya
upasuaji kwa aliyejeruhiwa lakini ghafla alisikia sauti ya mlipuko hatari na kombora la Hawen lilianguka juu ya kichwa chake na alianguka shahidi baada ya kuyaokoa maisha ya askari aliyejeruhiwa
Jina lake linaitwa juu ya Kituo cha reli katika kituo cha Elmaragha mkoani mwa Sohag na pia shule ya shahidi Elsayeh katika Elmaragha .Na kundi la kwanza linalohitimu kutoka Chuo cha matibabu cha Kijeshi kwa jina la Jenerali Daktari shahidi Muhamed Elsayeh Adly na pia hospitali ya chuo cha kijeshi kwa jina lake.
Ahmed El lawah ni Daktari wa kwanza aliyekufa kwa virusi vya Corona , yeye ni Profesa wa uchambuzi wa matibabu katika chuo kikuu cha Alazhar Na aliyeambukizwa na virusi vya Corona baada ya kuwasiliana na moja ya kesi zilizoambukizwa
Na yeye alitengwa nyumbani lakini hali yake ilizorota na alipelekwa hospitalini kwani hali yake ni hatari sana na aliwekwa kwenye Bomba la hewa.
Yeye alisumbua upungufu mkubwa wa kupumua na shinikizo kubwa la damu na baada ya hali yake iliboreshwa , alipelekwa karantini nyingine ,na ghafla kuzorota kutokea na alikufa siku ya Jumatatu.
Comments