Maelezo ya mkutano mdogo wa Rais El Sisi pamoja na idadi ya viongozi wa nchi za Afrika ili kujadiliana kuhusu matokeo ya ugonjwa wa Corona
- 2020-04-05 16:35:07
Jioni ya Ijumaa, Rais Abd El fatah El Sisi alishiriki katika mkutano mdogo kupitia mawasiliano na idadi ya viongozi wa nchi za kiafrika , pamoja na Rais mfaransa " ’Macron" , mkurugenzi mkuu wa shirika la Afya la ulimwengu ,ambapo mkutano umejumulisha Rais wa Jamhuri ya Afrika kusini , "Rais wa sasa wa umoja wa Afrika" , Marais wa Kenya , Mali, Congo ya demokarsia , Sengal , Rwanda , Zembabwi , waziri mkuu wa Ethiopia , pamoja na mkuu wa Kameshina ya Umoja wa Afrika na mkuu wa kituo cha Umoja wa Afrika kwa kupambana maradhi .
Msemaji rasmi kwa jina la Urais wa Jamhuri Balozi " Basem Rady " alisema kuwa mkutano mdogo umekuja ili kufuatilia matokeo ya mkutano uliopita kati ya viongozi wa Afrika ili kujadiliana kuhusu njia za kupambana na matokeo ya janga jipya la Corona katika nchi za kiafrika na kubainisha Vipaumbele vya bara ili kupambana virusi kwa uratibu na Jumuiya ya kimataifa , na majadiliano kuhusu matokeo ya mkutano wa kilele cha mwisho cha kundi la ishirini na kuratibu na nchi zake juu ya mahitaji za kiafrika katika upande huo .
Rais El Sisi alielezea kutoka upande wake uungaji mkono kwa yaliyotolewa katika tangazo la mkutano wa kundi la ishirini la mwisho uliotangazwa kwenye runinga ,akisisitiza umhimu wa kuendelea pamoja na nchi za kundi na washiriki wa kimataifa ili kutekeleza na kufaniyisha kilichokubaliwa ili kutoa msaada kwa nchi za kiafrika na kuziuunga mkono katika awamu hii maalumu , hasa kilichohusiana na ufadhili na kutoa msaada wa kifedha wa kimataifa ili kukabiliana na matatizo ya kiuchumi,kijamii na kiafya yanayosababishwa na janga la virusi vya Corona .
vilevile , Rais El Sisi alisisitiza umuhimu wa nchi za kiafrika kuongea kwa pamoja washiriki wa kimataifa na makampuni ya kifedha ya ulimwengu juu ya mlipuko wa janga la Corona ili kutilia mkazo vipaumbele vya ufanisi vinavyotimiza mahitaji ya bara kwa upesi ,na hivyo inafanyiwa katika mfumo wa kikazi kupitia Umoja wa Afrika na hilo linalokubaliwa na viongozi wa kiafrika .
pia Rais El Sisi alisisitiza tena kuwa kupamabana Atahri zilizosababishwa kutoka janga la Corona lazima kusambamba na juhudi za bara ili kukabiliana hatari za ugaidi zinazotisha Usalama na Utulivu wa nchi za kiafrika hasa eneo la pwani mwa Afrika .
Na wakati wa mkutano viongozi walikubaliana kuziita nchi za kiafrika zinazobaki ili kutoa misaada kwa kuimarisha sanduku la Umoja wa Afrika inavyowezekana kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona, liliidhinisha kuanzishwa wakati wa kilele kidogo cha kiafrika kilichopita, pia kusaidia juhudi zinazotolewa kwa kituo cha kiafrika kwa kupambana maradhi, pamoja na kuhimiza wajasiriamali waafrika na sekta binafsi ili kushiriki katika juhudi za kupambana na janga la virusi vya Corona barani Afrika, na kuainisha misaada ile katika mfumo wa shughuli za Umoja wa Afrika.
Pia ilikubaliwa suala la umuhimu wa kuimarisha uwezo wa Maabara na killiniki katika nchi za kiafrika ili kufanya vipimo kwa ajili ya kugandua virusi vipya vya Corona na kutosheleza njia za usalama kati ya nchi za bara ili kurahisisha harakati za bidhaa na vyombo vya matibabu vya dharura , pamoja na kuainisha utaratibu katika vituo vya kitaifa ili kupambana na majanga katika bara kwa lengo la kubadilishana Mazoezi na uzoefu , pamoja na kutoa mwito kwa Uchina ili kupa umuhimu kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za bara la Afrika katika upande huo .
Comments